Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo imekutana na kuzungumza na Menejimenti ya Shirika la Reli Tanzania (TRC) kuhusu Kanuni za Matumizi ya Miundombinu ya Reli kwa watoa Huduma Binafsi ya 2024, inayosimamiwa na Shirika hilo jijini Dar es Salaam 2 Agosti 2024.
Akizungumza mara baada ya mazungumzo hayo Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mheshimiwa Jasson Rweikiza ameipongeza Serikali kwa kutekeleza mradi mkubwa wa Reli ya Kisasa na kuruhusu kutungwa kwa Şheria inayoruhusu Sekta Binafsi kuwa na treni katika reli zote Mbili.
Mheshimiwa Rweikiza amesema uwepo wa Sheria hiyo na kanuni zake utaongeza ufanisi katika Uendeshaji wa reli hiyo na hivyo kuongeza ushindani katika uchukuzi.
Naye Naibu Waziri wa Uchukuzi David Kihenzile ameihakikishia Kamati kuwa Serikali itahakikisha kanuni hızo zinazingatia mahitaji halisi ili kuvutia wawekezaji wengi zaidi katika Uendeshaji wa reli.
Kaimu Mkurugenzi wa TRC ambaye pia ni Mkurugenzi wa Mitambo Mhandisi Albert Magandi amesema TRC iko katika hatua mbalimbali za kuhakikisha kanuni na nyaraka zinakamilika ili kuanza utelekelezaji wa Sheria hiyo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo Mh. Jasson Rweikiza akiongoza kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo pamoja na Menejimenti ya Shirika la Reli Tanzania (TRC) kuhusu Kanuni za Matumizi ya Miundombinu ya Reli kwa watoa Huduma Binafsi ya 2024 kilichofanyika makao makuu ya ya Shirika hilo JIJINI Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Uchukuzi David Kihenzile akitoa ufafanuzi baadhi ya maswali yaliyokuwa yanaulizwa na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo wakati wa kikao kilichokuwa kinajadili Kanuni za Matumizi ya Miundombinu ya Reli kwa watoa Huduma Binafsi ya 2024
Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo waliotembelea Shirika la Reli Tanzania (TRC)
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo wakiongozwa na Mwenyekiti Jasson Rweikiza pamoja na Naibu Waziri wa Uchukuzi David Kihenzile wakipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Huduma za Usafiri wa Reli Focus Sahani wakati wa ziara Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo Mh. Jasson Rweikiza akizungumza jambo alipotembelea kituo cha kuongozea treni ya umeme wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo
Naibu Waziri wa Uchukuzi David Kihenzile akizungumza jambo wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo ilipotembelea steisheni ya Dar es Salaam ya Shirika la Reli Tanzania (TRC)
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo wakiongozwa na Mwenyekiti Jasson Rweikiza pamoja na Naibu Waziri wa Uchukuzi David Kihenzile wakipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Huduma za Usafiri wa Reli Focus Sahani kuhusu ubira wa ujenzi wa Reli ya SGR wakati wa ziara Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...