Na Janeth Raphael- MichuziTv -Dodoma
Gavana wa Benk Kuu Tanzania (BOT) na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi ya Bima ya Amana (DIB) Emmanuel Tutuba amesema kuwa kiwango cha Mikopo Chechefu kimeshuka hadi kufikia asilimia 4.3 ikiwa ni kiwango cha chini kabisa ambacho kiko chini ya asilimia 5 inayokubalika Kimataifa.
Tutuba amesema hayo leo Jijini Dodoma Agost 7,2024 kwenye maonesho ya wakulima yanayoendelea katika viwanja vya nanenane Nzuguni na kueleza kuwa Tanzania Benk ziko salama kwa watu wote ambao wametunza fedha zao Benk.
"Lakini tunashukuru kwamba kiwango cha mikopo chechefu kimeshuka na sasahivi kiko asilimia 4.3 ikiwa ni kiwango cha chini kabisa ambacho kiko chini ya asilimia 5 inayokubalika Kimataifa".
"Kwahiyo sisi kama Tanzania benk zetu ziko salama kwa watu wote amabo wametunza fedha zao benk na tunaendelea kuwahakikishia kuwa viwango vinavyotumika kusimamia benk zetu ni viwango vya kimataifa kwahiyo kwa hivi karibuni hakuna benk itakayofilisika".
Aidha Gavana huyo amesema kuwa (DIB)ikiwa na jukumu muhimu katika usimamizi na udhibiti wa sekta ya bima nchini itaendelea kudhibiti , kusimamia na Kufuatilia kampuni zote za bima kuhakikisha zinazingatia sheria na kanuni ili kuweka viwango vya maadili na kuimarisha uwazi katika utendaji wa kampuni za bima.
Na kuongeza kuwa majukumu ya bodi hiyo ni kukagua na kutoa leseni kwa kampuni za bima ili kuhakikisha zinafaa kuendesha shughuli za bima.
Pia ametaja majukumu mengine kuwa ni pamoja na kutathmini Malalamiko kwa kupokea na kuyatatua kutoka kwa wateja kuhusu huduma za bima.
"Natoa wito kwa wananchi kutembelea banda la Bodi ya bima ya amana kujifunza zaidi, wanapaswa kuelewa kuwa tunaendeleza na kuboresha mazingira ya biashara ya bima kwa ajili ya kukuza ukuaji wa sekta hii ili kuhakikisha sekta ya bima inafanya kazi kwa ufanisi na kwa faida ya wateja".
" Sisi kama benki kuu tunaendelea kusimamia benki zisitetereke ambapo tupo katika mchakato wa kuboresha muundo wa kisheria na kiutendaji ili kuchangia kikamilifu na kwa kwa ubora na mchakato huu unalenga kuifanya Bodi ijitegemee kiutendaji".
Sambamba na hayo ameelezea ukubwa wa mfuko huo kuwa hadi kufikia June 30,2023 Mfuko wa bima ya amana ulikuwa na shilingi Trilioni 1.04 ambazo zimetokana na mchango wa Serikali wa shilingi Bilioni 1.05 ambazo zilitolewa wakati wa kuanzisha mfuko mwaka 1994 na kufafanua kuwa hadi kufikia June 30,2024 mfuko ulikuwa na wanachama 44.
Mbali na hayo ameeleza muundo wa Bodi hiyo kuwa upimo chini ya Mamlaka ya Bodi ya wakurugenzi ambayo ina jukumu la kuunda Sera na kuhakikisha utawala bora.
"Kwa mujibu wa Sheria iliyounda bodi ya bima ya amana, Bodi ya wakurugenzi ya bodi ya amana imejumuisha wajumbe wanaotoka BoT ambaye ni Gavana, Mwakilishi wa wizara ya fedha, Katibu Mkuu wizara ya fedha na Wajumbe wengine watatu wanaochaguliwa na Waziri wa fedha".
Ikumbukwe kuwa DIB ni Taasisi iliyoanzishwa kwa mujibu wa Sheria ya benki na Taasisi za fedha ya mwaka 1991 ambapo ilianza kufanya kazi zake mwaka 1994 chini ya usimamizi wa BOT.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...