Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam. Jumla ya mashabiki nane wa soka watapara fursa ya kutembelea nchini Dubaiendapo watashinda tiketi kupitia promosheni ya Dubai Kumenoga ilitoziduliwa na kampuni ya michezo ya kubahatisha Parimatch kwa kushirikiana na Airtel Tanzania kupitia huduma za Airtel Money.
Promosheni hiyo ni muendelezo wa kampeni kubwa iliyomalizika ya Zigo la Euro 2024 nchini Ujerumani ambapo mashabiki wa soka walishinda zawadi mbalimbali.
Meneja Masoko wa Parimatch, Levis Paul amesema kuwa dhumuni kubwa ya promosheni hiyo ni kuwapa wateja wa Parimatch thamani na kukata kiu ya ndoto za watanzania wanaotamani kusafiri kwenda Dubai kwa mapumziko.
“Promosheni hiii ni mahususi kwa wateja wetu wote wa Parimatch na wanaotumia mtandao wa Airtel Money wenye akaunti na hata wateja wapya watakaojiunga kw sasa.
Lengo letu ni kuwawezesha kuendelea kucheza na kufurahia burudani kabambe za falme za kiarabu (Dubai). Kuanzia Agosti 7 mpaka Oktoba 6, mteja wa Parimatch akifanya ubashiri wake kwenye mchezo wowote wa soka kupitia tovuti www.parimatch.co.tz au App yetu ataingia kwenye droo na kuweza kushinda tiketi,” alisema Levis.
Alisema kuwa vile vile kwa asiyekuwa mteja wao anaweza kushiriki kwa kujisajili kupitia www.parimatch.co.tz na kuweka pesa kupitia airtel money na kuweka ubashiri katika mechi yeyote. Kadri unavyoweka beti zaidi ndivyo unajiongezea nafasi ya kujishindia tiketi ya kwenda Dubai au kujishindia pesa taslimu kiasi cha Sh50,000 kila siku hadi Sh200,000” alisema Levis.
Levis pia alisema kuwa mteja anaweza kujisajili kupitia menu ya Airtel Money, mteja anaweza kufuata njia hizi ili kuweza kuweka pesa yake na kuanza kusuka mkeka wa ushindi *150*60# kisha namba 4 lipa bill, weka code za 351144 unaweza kuweka pesa na kushinda kushinda safari ya kwenda Dubai au pesa taslimu kutoka katika droo ya siku husika ya promosheni
Pamoja na hayo, Levis amewataka Watanzania kiujumla kuchangamkia fursa hiyo ya kipekee kwa kubeti na Parimatch ili wawe miongoni mwa washindi watakaobahatika kujishindia safari ya kupelekwa Dubai na Parimatch kula bata huku gharama zote zikiwa zimelipiwa.
Kampuni ya Parimatch ndio kinara wa michezo ya kubashiri mtandaoni na imekuwa ikitoa ofa kubwa ya bonasi ya Ukaribisho ya 125% hadi kufikia TZs 1,000,000 kwa wateja wapya wanaojiunga nao!
Parimatch imekuwa ikifanya kazi nchini Tanzania tangu mwaka 2019, ikitoa huduma nzuri ikijumuisha malipo ya haraka, odds kubwa na promosheni za kusisimua kwenye soka, Kasino na Michezo ya virtual. Mbali na soka, kampuni ya Parimatch pia hutoa mamia ya matukio kila siku kwenye tenisi, UFC, mpira wa vikapu, Kriketi, baseball na michezo mingine mingi ya Live na pre-match.
Meneja Masoko wa kampuni ya michezo ya kubashiri ya Parimatch, Levis Paul (wa pili kulia) akizungumza wakati wa uzinduzi wa promosheni ya Dubai Kumenoga iliyozinduliwa kwa kushirikiana na kampuni ya ya simu ya Airtel kupitia huduma za Airtel Money ambapo jumla ya washindi nane watashinda tiketi na kupata fursa ya kutembelea nchini Dubai. Wa kwanza kulia ni balozi wa kampuni ya Parimatch, Haji Manara na maofisa wengine wa Airtel ambao ni , George Majumba (wa tatu kushoto), Chakicha Mshana ( wa pili kushoto) na balozi wa Parimatch, Ester Luckson maarufu kwa jina la Mama Chanja wa kwanza kushoto.
Meneja Masoko wa kampuni ya michezo ya kubashiri ya Parimatch, Levis Paul (kulia) akipongezana na mmoja wa maofisa wa kampuni ya mtandao wa simu ya Airtel wa kitengo cha Airtel Money, George Majumba wakati wa uzinduzi wa promosheni ya Dubai Kumenoga ambayo itawawezesha jumla ya washindi nane kutembelea nchini Dubai
Mkurugenzi wa kampuni ya michezo ya kubashiri ya Parimatch, Eric Gelard (wa pilu kulia) na meneja masoko, Levis Paul wakiwa katika picha ya pamoja na mabalozi mbalimbali wa kampuni hiyo wakiongozwa na Haji Manara ( wa tatu kushoto) wakati wa uzinduzi wa promosheni ya Dubai Kumenoga ambayo itawawezesha jumla ya washindi nane kutembelea nchini Dubai. Wengine katika picha ni Asma Majid “Silivestery” (wa pili kulia), Vicent Njau ‘Kiredio’ ( wa kwanza kulia) na Ester Luckson “Mama Chanja” wa pili kushoto.
Mkurugenzi wa kampuni ya michezo ya kubashiri ya Parimatch, Eric Gelard akifuatilia kwa makini uzinduzi rasmi wa promosheni ya Dubai Kumenoga ambayo itawawezesha jumla ya washindi nane kutembelea nchini Dubai. Parimatch imeshirikiana na kampuni ya simu ya Airtel kupitia kitengo cha Airtel Money kuendesha promosheni hiyo ambapo jumla ya washindi nane watapata fursa ya kutembelea nchini Dubai.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...