ALIYEKUWA Mbunge wa Iringa Mjini kwa tiketi ya CHADEMA kwa kipindi Cha miaka 10 Mchungaji Peter Msigwa ambaye kwa sasa amejiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) ameendelea 'kukivua nguo' chama chake Cha zamani kwa kuanika madudu yao hadharani.
Mchungaji Peter Msigwa ambaye yuko katika ziara ya Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi ( CCM) Mkoa wa Dar es Salaam , Mchungaji Msigwa amesema amekuwa CHADEMA na kazi yao ni kupinga maendeleo yanayofanywa na Serikali inayoongozwa na Rais Dk.Samia Suluhu Hassan.
"Wapinzani wamepoteza dira hawajui wanaenda wapi ,hawana muelekeo wowote lakini Rais Samia anamuelekeo na anakwenda katika uelekeo sahihi.CHADEMA na vyama vingine vya upinzani vimepotea ,vinatia hofu lakini Rais Samia anatia tumaini.
Amesema Wananchi wasikubali kudanganywa na wapinzani maana hawana lolote wanaloweza kufanya kwa ajili ya kuleta maendeleo na wenyewe wanajua hawana uwezo huku akifafanua viongozi wote wenye akili wameendelea kuikimbia CHADEMA akiwemo yeye mwenyewe.
Amesema Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe amekuwa aking'ang'ania madaraka na hataki kuachia nafasi kwa wengine,nafasi zote anataka kushika yeye na kutoa mfano kuwa Mbowe ni kama Nkurunzinza.
Akizungumza uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan tangu alipoingia madarakani, Mchungaji Msigwa amesema Rais amejibu maswali ya wananchi katika nyanja mbalimbali.
Alisema wananchi walikuwa na swali kuhusu ukuaji wa uchumi lakini Rais Samia amejibu swali hilo kwani uchumi katika kipindi cha miaka mitatu umeongezeka kutoka asilimia nne mpaka asilimia tano.
Swali kingine la wananchi kilikuwa linahusu kurejea umoja na mshikamano na katika hilo Rais Samia amekuja na maridhiano kupitia R4 na kufafanua Rais anataka Watanzania wawe wamoja.
"Nchi yetu ina maridhiano na sisi ni ndugu tukae pamoja.Tulipokuwa tunataka mikutano Rais akaruhusu na tulipoenda katika mikutano watu hawatusikilizi tukasema tunataka maandamana rais akaruhusu maandamano mwisho wa siku tunabakia kuambiwa na Mbowe kunja ngumi.
"Swali la tatu kwa Rais kilikuwa nchi yetu kutokuwa na mahusiano na nchi nyingine ,tulikuwa tuko katika kisiwa lakini Rais Samia amefungua nchi, wawekezaji wanakuja kwa wingi. Takwimu zilizopo zinaonesha miradi zaidi ya 3000 imesajiliwa TIC.
"Watalii walikuwa 1500,000 lakini wameongeza mpaka kufikia 1800,000 na mapato yameongezeka.Tulikuwa Kigoma tumeelezwa Rais Samia amepeleka fedha Sh.trilioni 11.4 kwa ajili ya miradi ya maendeleo
"Mkoa wa Kagera Rais amepeleka fedha Sh.trilioni 12 kwa ajili ya miradi ya maendeleo.Mwanza ndio funga kazi kabisa maana Rais amepeleka fedha nyingi.CHADEMA tumekuwa tukipinga kila kitu,na usipopinga unaadhibiwa.
"Ukurasa wa 72 wa CHADEMA umezungumza kuhusu kuboresha bandari lakini baada ya Serikali kuamua kuboresha Bandari wakaanza kumpinga Rais Samia.CHADEMA hawana nia,hawana uwezo, hawawezi kuwapeleka kokote.
"Naomba Watanzania tumuuonge mkono Rais Samia kwani analipeleka Taifa mahali panapostahili."amesema Mchungaji Msigwa alipokuwa akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika Temeke Azimio.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...