Mtoto Mchanga ameokolewa na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Jijini Dodoma baada ya mama yake aitwae Catherine Iwaho kumtupa mtoto huyo chooni. Mara baada ya mtoto huyo kuokolewa alikimbizwa Hospitali ya Mkoa wa Dodoma (General) kwa Matibabu zaidi Agosti 26, 2024

Tukio Hilo limetokea maeneo ya Ipagala ambapo mtoto huyo amekutwa akiwa hai. Akitoa taarifa ya tukio hilo Mkaguzi Deogratius Inano amesema Baada ya kuvunja sehemu ya choo hicho majira ya Asubuhi walikumkuta mtoto huyo.

Aidha, Naibu Kamishna Puyo Nzalayaimisi akiambatana na Kaimu Kamanda Mkoa wa Dodoma Mrakibu Rehema Menda wamemtembelea na Kumjulia hali Mtoto huyo ambaye anaendelea na Matibabu katika Hospitali hiyo ya Rufaa ya Mkoa

"Sisi Jeshi la Zimamoto tunakemea na kulaani Vikali kabisa juu ya suala hili la kutupa watoto chooni au kwenye mashimo ya taka, kila mtu anahaki ya kuishi kama Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inavyoelekeza" amesema DCF Nzalayaimisi



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...