Na Chalila Kibuda,Dodoma
Tume ya Taifa ya Umwagiliaji(NIRC) imesema sheria ya umwagiliaji imewekwa katika kuondoa changamoto zinazoikabili sekta ya umwagiliaji nchini.
Akizungumza leo kwenye maonesho ya Kimataifa ya wakulima yanayoendelea kwenye viwanja vya Nanenane Nzuguni Jijini Dodoma Afisa Sheria mwandamizi NIRC Amina Mweta amesema kumekuwa na ushiriki mdogo wa wakulima na sekta binafsi katika kuendeleza kilimo cha umwagiliaji ni chanzo cha uanzishwaji wa sheria hiyo itayofanya shughuli za umwagiliaji kuwa endelevu nchini kutokana na uzalishaji wa Sekta hiyo.
"Sheria ya Taifa ya umwagiliaji na.4 ya mwaka 2013 imetugwa na kupitishwa na bunge mwaka 2013 ikatiwa saini na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan Oktoba 20,2013 sheria hii imeanzishwa na Tume ya Umwagiliaji ili kusimamia kilimo cha umwagiliaji na kutatua changamoto za wakulima",Amesema.
Ameongeza kuwa sababu nyingine ya kuanzishwa sheria hiyo ni pamoja udhaifu wa mifumo ya kitaasisi ambao ulikua haukidhi kasi ya kuendeleza kilimo cha umwagiliaji lakini pia uvamizi wa maeneo ya ardhi yanayofaa kwa kilimo cha umwagiliaji.
Sambamba na hayo amebainisha vitendo vilivyokatazwa katika sheria ambapo ni pamoja na kuingia katika ardhi ya umwagiliaji kwa madhumini tofauti na umwagiliaji.
Amesema ,kuruhusu sumu ya viwandani au uchafu wa majumbani kuingia kwenye skimu yeyote ya umwagiliaji bila kutibu maji kikamilifu kunaua uoto wa asili pamoja na umwagiliaji huo kukosa tija kwa Taifa.
Aidha amesema kutokana na hali iliyokuwepo na changamoto ambazo zimeikabili sekta ya umwagiliaji sheria imesaidia kuongezeka kwa mchango wa umwagiliaji katika uzalishaji wa chakula na lishe lakini pia kuongezeka kwa pato la wakulima na Taifa kwa ujumla.
Naye Mhandisi Mwandamizi wa Umwagiliaji Naomi Mcharo amesema kwa mwaka huu wa fedha NIRC wamejipanga kuchimba visima 1000 nchi nzima.
Aidha amesema NIRC wanaendelea na miradi mbalimbali ya umwagiliaji nchini ili kuhakikisha kilimo cha umwagiliaji kinakuwa na kumnufaisha mkulima.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...