Na Oscar Assenga, TANGA

MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) wa zamani Profesa Mussa Assad amesema ni umuhimu kuwepo kwa ushirikiano wa pamoja ili kuhakikisha ujenzi wa Hospitali ya Kiislamu Mkoani Tanga unakamilika kwa wakati na kuanza kutoa huduma.

Profesa Assad aliyasema hayo mwishoni mwa wiki Jijini Tanga wakati aliposhiriki kwenye Kongamano la tathimini ujenzi wa Hospitali ya Kiislamu Mkoa wa Tanga lililokwenda sambamba na kufanyika kwa harambee ya kuchangia ujenzi wake huku akieleza ni ushirikiano ni lazima wawe wamoja katika kufanikisha hilo.

Harambee hiyo ilikwenda sambamba na uliokwenda sambamba na kukagua eneo la Ujenzi wa Hospitali hiyo lililopo Kata ya Masiwani, Kupanda miti ya Matunda pamoja na kuweka jiwe la Msingi.

Alisema kwa sababu jambo ambalo linafanyika ni la kuokoa maisha na ukiokoa maisha ya mtu mmoja utakuwa umeokoa maisha ya watu wote kwani hata vitabu vitakatifu vya Mungu (Quran) vimeandikwa hilo.

“Hata vitabu vitakatifu vya Mwenyezi Mungu vinaeleza kumtibu mtu mmoja na kuyaokoa maisha yake ni sawa utakuwa umeuokoa umma nzima lakini tatizo ambalo analiona ni ajizi kwamba wanafikiria hawawezi leo kufanya jambo hilo labda wasubiri kesho itawezakena na mwisho miaka inapita anzeni sasa”Alisema.

“Hilo ni tatizo kubwa la ajizi hivyo tuondoe ajizi tulifanye kazi hi kwa ushirikiano mkubwa ili kuweza kutimiza malengo tuliojiwekea ya kuhakikisha ujenzi wa eneo hilo unaendelea “Alisema

“Leo nimefurahi kwa sababu kuna kazi kubwa imefanywa na amesikitika hatua zake zimekwenda taratibu mno na nimekuwa nikipita sana kwenye eneo hilo kila mwezi kwenda Tongoni na wala sijasikia kuwepo wa shughuli hizi pia kinachomsikitisha zaidi ni kumetolewa nondo 72 katika ujenzi huu”Alisema

Aidha alisema maana yake hawajali vitu vyao wenyewe hivyo ni wajibu wao kuhakikisha wakifanya vitu hapo vilindwa ili kuepusha kuibiwa na wezi jambo ambalo litapelekea kuepukana na vitendo hivyo.

“Lakini niwasihi katika jambo hilo tuwe pamoja na kuongeza mshikamano ili kulifanikisha jambo hilo na mwakani mungu akipenda kutakuwa wamepandisha jengo pia tutaendelea kuona namna wadau mbalimbali wanaweza kuchangia kwenye ujenzi huu”Alisema

Kwa makadirio ya Fedha za ujenzi wa Hosptali hiyo unakadiriwa kuwa ni zaidi ya Sh.Bilioni 2.4 sio fedha ndogo hivyo ni lazima waone namna ya wao wenyewe wajipange wafanya juhudi kubwa za kuanza kazi hiyo na wao waanze wenyewe na wao watakaoona hivyo wanaweza kuona namna ya wadau wengine kuwaunga mkono.

“Lakini niwaambie kwamba Mwenyezi Mungu akijalia nikirudi Dar nitahamasisha wenzangu kuona namna nzuri ya kuliendelea jengo hlo lianze haraka sana kutokana na umuhimu mkubwa lilikokuwa nalo”Alisema

Alisema kwamba Mwenyezi Mungu amewajalia neema nyingi waislamu hivyo ni vema wajiulize wameifanyia nini hiyo neema ya umri wamekaa miaka miwili jengo hilo hivyo maana yake wamefanya ajizi na hawakufanya hima ya kutekeleza kazi hiyo.

“Jambo la muhimu ni kujikumbusha kwamba tumepewa neema ya umri siku zinavyokwenda tujipime namna gani tumefanya kazi hizo inshallah Mwenyezi Mungu ajalie tukae pamoja juhudi hizi ziendelezwe ili mwakani tusiwe na msingi tuwe tumepanda kama sio ghorofa moja itakuwa ghorofa mbili na hilo tutaliweza kama tutakuwa wamoja”Alisema

Awali akizungumza kuhusu mradi huo wa Ujenzi wa Hospitali inayozingatia maadili ya Kiislamu Mjumbe wa Halmashauri Kuu wa Baraza la Waislamu Taifa (Bakwata) Sheikh Khamis Mataka alisema kwamba MwenyeziMungu atalipa nguvu jambo hilo ili litimie na uwezo huo wanao.

Alisema kwamba uwezo wa kulitimiza jambo hilo upo ndani yao wao wenyewe wakiondokana na matatizo na changamoto walizojiwekea wao wenyewe wataona namna suala hilo litakavyopata mafanikio.

Naye kwa upande wake Dkt Ally Fungo alisema kwamba mradi huo wa kimkakati umedhamiria kutatua tatizo la kimkakati kama halitatatuliwa litaadhidhiri dhamira ya jamii ya kiislamu kwa kwa maana hapo watakuwa na kituo cha afya cha kutoka tiba kinachzingtia maadili ya kiislamu ambayo ni ya kibinadamu.

Alisema kwamba hospitali hiyo haitakuwa ya waislamu pekee bali wote lakini haiwezekani wakina mama wakatibiwa na daktari mwanaume hiyo ni hospitali ya kimkakati kutatua kimkakati hospitali ya waislamu wenyewe kwa fedha zao wenyewe.

“Hospitali hii itakuwa na majengo sana kuanzia Jengo la Utawala ,Jengo la Madaktari,Wodi za Wakina Mama,Kina Baba ,Maabara,Mochwari ,na nyenginezo na gharama zake kwa awali tungetumia Bilioni 1.5 lakini kipindi kimepita miaka mitatu iliyopita”Alisema

Hata hivyo alisema kutokana na uchumi duniani kuadhirika hivyo sasa wamefanya ufuatiliaji vitu vimebadilika na bei ya vitu imeongezeka na hivyo watalazimika watumie bilioni 2.4 hilo sio jambo dogo ni kubwa hivyo watashirikiana na wadau wote kufanikisha hilo.













Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...