Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) inaendesha mafunzo kuhusu Sheria na Kanuni mpya za Ununuzi wa Umma kwa Menejimenti, Wajumbe wa Bodi ya Zabuni na wataalam wa kitengo cha Ununuzi na Ugavi kutoka ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali yanayofanyika kwa siku tano kuanzia Agosti 19 hadi Agosti 23, 2024.
Akizungumza na Michuzi Blog Mkurugenzi wa Maendeleo ya Taaluma kutoka Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) Amos Kazinza amesema kuwa mafunzo hayo ni muhimu sana kwani yanaleta uelewa wa pamoja kwa watekelezaji wa sheria kuhusu mabadiliko muhimu yaliyopo kwenye sheria na kanuni mpya
Amesema Sheria na kanuni mpya zimelenga kuleta ufanisi mkubwa katika utekelezaji wa myororo wa Ununuzi na Ugavi.
Aidha mambo ya muhimu yaliyopo kwenye ni kuwepo kwa viwango vya ukomo wa uidhinishaji wa zabuni kwa Bodi ya zabuni na afisa Masuuli, kufungamanisha masuala ya mnyororo wa ugavi kwenye sheria za ununuzi wa umma, kuweka utaratibu utakaozungatiwa na Taasisi za Umma zinazojiendesha kibiashara katika ununuzi.
Pia amesisitiza kuwa ni kuweka sharti la bei ya kikomo katika sheria ya ununuzi wa umma, Taasisi ununuzi kutoa upendeleo kwa wazabuni wa ndani katika zabuni za bidhaa, ujenzi na huduma, Uwasilishwaji wa taarifa ya tathmini ya utendaji wa kazi za ununuzi wa umma na thamani halisi ya fedha kwa Rais kila ifikapo au kalba ya tarehe 30 Marchi kila mwaka na kupunguza muda wa mchakato
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...