Wagonjwa wenye changamoto ya figo wanaohitaji kupandikizwa figo ambayo ni tiba stahiki kwa wagonjwa wanaosafisha damu na hawana uwezo wa kulipia gharama za upandikizaji watahudumiwa kupitia fedha alizotoa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa Hospitali ya Taifa Muhimbili ili ziweze kufanya kazi hiyo.

Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Prof. Mohamed Janabi wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya wachangia viungo duniani ambayo hufanyika kila mwaka tarehe 13 Agosti na kuhudhuriwa na wananchi waliopandikizwa figo pamoja na wenzao waliowachangia figo.

Prof. Janabi amesema kwa sasa wanatafuta seti ya wagonjwa 10 na ndugu zao 10 ambao wapo tayari kuwachangia figo na watakapokidhi vigezo husika watanufaika na huduma hiyo.

Amesema Tanzania ni miongoni mwa nchi tisa zilizopo Kusini mwa Jangwa la Sahara zinazopandikiza figo Barani Afrika ambapo katika kipindi cha miaka saba tangu kuanzishwa huduma hiyo nchini, wagonjwa 102 wameishapandikizwa kupitia kampasi mbili za Upanga na Mloganzila.

 Kwa upande wake mmoja wa wachangia figo Bw. Juma Kanzaga ambaye alichangia figo akiwa na umri wa miaka 70, amewashukuru wataalam wote wa hospitali kwa kazi nzuri wanayofanya na kutoa wito kwa watanzania kuendelea kujitoa kuwachangia ndugu zao wenye uhitaji wa kupandikizwa figo.






 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...