Na Munir Shemweta, WANMM BAHI

Serikali itafuatilia madai ya wananchi wa wilaya ya Bahi mkoani Dodoma kutakiwa kuwa na mawakili wakati wa kusikilizwa mashauri ya ardhi kwenye Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya wilaya.

Hayo yameelezwa tarehe 19 Agosti 2024 na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi mhe, Geophrey Pinda katika mkutano wa hadhara kwenye kijiji cha Ibihwa wilaya ya Bahi wakati wa ziara ya Makamu wa Rais mhe. Dkt Philip Mpango kukagua shughuli za maendeleo mkoani Dodoma.

"Nataka nitoe maelekezo rasmi kwa wenyeviti wote wa Mabaraza ya Ardhi kwamba mwananchi anaruhusiwa kuendesha kesi yeye mwenyewe au kuweka wakili wala siyo jambo la kikanuni kuwa kila mwenye tatizo lazima awe na wakili". amesema Mhe. Pinda

Kauli ya mhe. Pinda inafuatia maelezo ya mbunge wa jimbo la Bahi mhe. Kenneth Nollo kuwa, wananchi wanaopeleka mashauri kwenye Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya wanatakiwa kuwa na mawakili wa kuwatetea wakati wa kusikilizwa mashauri yao kwenye mabaraza hayo.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda akizungumza katika mkutano wa hadhara katika kijiji cha Ibihwa wilayani Bahi mkoa wa Dodoma wakati wa ziara ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Philip Mpango tarehe 19 Agosti 2024.


Sehemu ya wananchi waliohudhuria mkutano wa Makamu wa Rais Mhe. Dkt Phillip Mpango wakati wa ziara yake mkoani Dodoma tarehe 19 Agosti 2024.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Philip Mpango akisalimiana na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda alipowasili kijiji cha Ibihwa wilayani Bahi mkoa wa Dodoma tarehe 19 Agosti 2024.
 
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda akizungumza na Mkuu wa Mkuu wa mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule katika kijiji cha Ibihwa wilayani Bahi mkoa wa Dodoma wakati wa ziara ya Makamu wa Rais Mhe. Dkt Philip Mpango tarehe 19 Agosti 2024. (PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...