NA WILLIUM PAUL, SAME.
BAADHI ya Wananchi wa Kata ya Kalemawe Wilayani Same (Jimbo la Same Mashariki) wameiomba Serikali kuboresha Sheria ya kiwango cha fidia (kifuta machozi) kinachotolewa kwa waathirika wa uvamizi wa Wanyama wakali na waharibifu (Tembo) ambao wamekuwa kero kubwa kwenye maeneo yao.
Wameeleza hayo kwenye mkutano wa hadhara wa Mkuu wa Wilaya ya Same Kasilda Mgeni ambapo wamesema kiwango kinachotolewa kwa sasa hakiendani kabisa na athari zitokanazo na Wanyama hao pindi wanapovamia mashamba yao.
Akitolea ufafanuzi wa malalamiko ya Wananchi hao Mkuu huyo wa Wilaya amesema kuwa sheria hiyo imebadilishwa tayari na kwa wale Wananchi ambao mazao yao yaliharibiwa kwa kipindi cha mwaka 2023/24 Serikali ikija kuanza kulipa fidia (kifuta machozi) itaanza kutumika sheria mpya na siyo ile ya zamani.
Sambamba na hilo katika mwaka wa fedha 2024/25 kuna kituo cha kufuatilia mwenendo wa Wanyama hao pindi wanapotoka kwenye hifadhi ili askari waweze kuwadhibiti kabla ya kuleta madhara kwenye jamii”
Adha amesisitiza Wananchi kuwa, Serikali imekuwa ikitumia mbinu mbalimbali za kukabiliana na Wanyama hao ikiwemo kutoa mafuzno kwa vijana (Askari wa Wanyama pori vijijini VGS) ya matumizi ya vifaa vya kufukuzia Tembo kwenye kila jamii zinazozunguka Hifadhi hivyo utaratibu huo unapofika kwenye jamii zao wajitokeze kwa wingi kupata hiyo elimu itawasaidia kujikinga na madhara yatokanayo na uvamizi wa Wanyama hao.
Pia Kasilda amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia Wizara ya Maliasaili na Utalii kwa jitihada zake za dhati za kutatua changamoto ya Wanyama pori waharibifu wa mazao ya binadamu yaani Tembo ambao wamekuwa kero kubwa kwa Wananchi wa Same wanaozunguka hifadhi ya Taifa ya Mkomazi,
Pia amempongeza Mbunge wa Jimbo la Same Mashariki mama Anne Kilango, akisema matokeo ambayo yanaonekana leo hii juu ya changamoto hiyo ni jitihada zake ambazo amezifanya akiwa Bungeni kusimama vyema kwenye nafasi yake ya uwakilishi wa wananchi kulisemea jambo hilo hali ambayo imefanya Serikali kusikia hoja zake na kuzifanyia kazi kwa vitendo.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...