Na WAF - MWANZA

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Saidi Mtanda amewataka watoa huduma za afya kwa njia ya tiba asili nchini kushirikiana na Serikali kukemea na kutokomeza vitendo vya ukatili ndani ya jamii.

Mtanda ametoa kauli hiyo Agosti 28, 2024 wakati akifungua juma la tiba asili na maadhimisho ya tiba asili kwa Mwafrika yanayofanyika kwenye viwanja vya Furahisha Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza.

"Waganga wa tiba asili mna mchango mkubwa katika kuimarisha afya za watanzania, hivyo tukiunganisha matumizi ya dawa zenu na zile za hospitalini wananchi watastawi kwa kuwa na afya njema". Amesema Mhe. Mtanda na kuongeza.

"Ni rai yangu wote tuungane kutokomeza vitendo vya ukatili wa mauaji ya Albino na watoto ambayo yamekuwa yakiripotiwa hivi karibuni". Amesisitiza Mtanda.

Aidha, Mtanda ametumia fursa hiyo kuwataka waganga wa tiba asili nchini kujisajili kwenye baraza la tiba asili na mbadala na kuhuisha leseni zao kila mwaka ili kuepuka kukumbwa na mkono sheria.

"Mimi ninaamini tiba hizi za asili zinapoboreshwa zinafanya kazi sawa na tiba hizi za kawaida na ndio maana Watanzania zaidi ya asilimia 60 wanatumia tiba hizi na zinawasaidia, wote tunatambua kwamba tiba asili na tiba mbadala zimekuwa na mchango mkubwa kwa wananchi na ofisi ya mkuu wa mkoa kupitia sekta ya afya". Amesema Mkuu wa Mkoa huyo.

Kwa upande wake Mwenyekiti msaidizi baraza la tiba asili na mbadala nchini Dkt. Elizabeth Lema amesema waganga wa tiba hizo wametoka kwenye mfumo wa kufanya kazi zao kienyeji na sasa wanafanya kisasa na wakati mwingine wanatoa huduma jumuishi na wataalamu kutoka hospitali za kawaida ambao wanakiri kwamba tiba za asili zinamsaada mkubwa katika kutibu magonjwa mbalimbali.

Naye Msajili wa baraza la tiba asili na mbadala Martin Mgogwa amebainisha kuwa baraza hilo pamoja na kuwasajili linasimamia, kuthibiti na kuendeleza tiba asili nchini kwa kuhakikisha kila anayetoa huduma za tiba asili anasajiliwa pamoja na kuhuisha leseni kila mwaka katika eneo lake.

Akizungumza katika hafla hiyo ya ufunguzi Meneja wa Kanda ya ziwa wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia mkuu wa Serikali ametoa wito kwa wadau kuhakikisha wanafika kwenye ofisi hizo ili dawa wanazotumia ziweze kuchunguzwa kama zina kemikali dawa badala ya kuwa na sumu.

Maadhimisho hayo ya tiba asilia ya Mwafrika yaliyoanza tangu Agosti 25 mpaka Agosti 31 yana lengo la kusimamia utoaji huduma bora na salama za tiba asili kupitia mifumo sahihi ya udhibiti.


















Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...