MOSHI.

BAADHI ya Watu Wenye Ulemavu mkoani Kilimanjaro wamemshukuru Mbunge wa Viti Maalum kundi la Watu Wenye Ulemavu na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu, Ummy Nderiananga kwa moyo wake wa kujitoa kuwahudumia watu wenye ulemavu.

Wakizungumza mara baada ya mkutano wa ndani uliofanyika katika Tarafa ya Vunjo Mashariki, wilaya Moshi ikiwa ni muendelezo wa ziara yake katika mkoa huo wamesema wamekuwa wakipokea misaada ya vifaa saidizi vikiwemo viti mwendo na fimbo nyeupe kwa wasioona kutoka kwa Mbunge huyo vinavyowasaidia kufanya shughuli zao.

Akizungumza baada ya mkutano huo mkazi wa Njiapanda mwenye ulemavu Flora Ngowi aliipongeza Serikali kwa kuendelea kupaza sauti kukemea vitendo vya baadhi ya watu wanaowaficha watu wenye ulemavu ndani akisema vitendo hivyo huwanyima fursa ya kushiriki katika shughuli za maendeleo.

Pia mkazi wa Tarafa ya Vunjo Mashariki mwenye mtoto mwenye ulemavu Sabina Mazengo aliishukuru Serikali kwa kuweka miundombinu rafiki inayoweza kutumiwa katika majengo na mahali penye huduma za kijamii kama hospitali, masoko, vituo vya Daladala na shule kwa ajili ya wanafunzi wenye mahitaji maalum.

Kwa upande wake Mbunge wa Viti Maalum kundi la watu wenye ulemavu na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Ummy Nderiananga aliwapongeza kwa kuendelea kuwatunza watoto hao akisema Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan alitoa fedha za ujenzi wa mabweni 80 Nchi nzima kwa ajili ya watoto wenye ulemavu waweze kusoma katika mazingira rafiki na salama.

Aidha Nderiananga alikabidhi mifuko ya saruji 100 kwa ajili ya ujenzi wa msikiti wa Masjid Mussa uliopo katika Tarafa ya Hai Mashariki, Kata ya Mabogini mkoani Kilimanjaro.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...