Na Mwandishi Wetu
MAKAMU wa Rais Dkt.Philip Mpango amesema uwekezaji unaofanywa na Serikali katika sekta ya imwagiliaji unaenda kuandika historia ya kumaliza tatizo la njaa nchini na kulijengea Taifa heshima kupitia uwepo wa chakula cha kutosha.
Amesema anaridhishwa na kazi kubwa inayofanywa na Tume ya Taifa ya Umwagiliaji chini ya Wizara ya kilimo hivyo wananchi wawe tayari kuipokea miradi hiyo mikubwa sekta ya umwagiliaji itakayomaliza tatizo la uhaba wa chakula na kuimarisha kilimo cha uhakika nchini.
Ameyasema hayo alipokuwa akizungumza wakati wa ziara yake mkoani Dodoma iliyokwenda sambamba na uwekaji wa jiwe la Msingi katika ujenzi wa Shamba la Pamoja la Dkt. Samia Suluhu Hassan (Dkt Samia Suluhu Hassan Block Farm) unaotekelezwa na Tume ya Taifa ya Umwagiliaji ukiwa na thamani ya zaidi ya Sh.bilioni 21.7
“Hapa Dodoma kuna salamu ya Mkuliachi ambayo ni salamu na inamaanisha njaa, niwahakikishie kuwa hiyo salamu inaenda kuisha kupitia uwekezaji unafanywa na serikali katika miradi hii mikubwa ya umwagiliaji inaenda kuandika historia ya kumaliza tatizo la njaa nchini na kulijengea Taifa heshima ya uwepo wa chakula cha kutosha.
“Niwashukuru wananchi wa maeneo ya mradi kwa kuridhia kutoa ardhi yao na kazi kubwa inayofanywa na Tume chini ya Wizara ya kilimo katika kufanikisha miradi hii,”alisema.
Pia amesisitiza Tume ya Taifa ya umwagiliaji, na inafanya kazi kubwa na hatua hiyo ndio maana ya kubadili mifumo sekta ya kilimo na kuwa na kilimo chenye tija na cha uhakika.“Nawapongeza sana,hili litakuwa ni eneo la mfano na mashamba haya yawe mashamba darasa,elimu ya Kilimo itolewe hadi kwa vijana hususani vitendo siyo maneno”
Dkt.Mpango ametumia nafasi hiyo kusifu hatua ya mradi huo kuhusisha ujenzi wa kituo cha afya na barabara yenye urefu wa zaidi ya kilomita 18.8 umbapo ujenzi huo unatekelezwa na Tume ya Taifa ya Umwagiliaji.
Ameagiza eneo la barabara lililobaki ambalo lipo chini ya Wakala wa Barabara Vijijini (TARURA) litekelezwe na Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) na kuwapo na miundo mbinu ya uhakika ya mawasiliano katika vijiji hivyo vya mradi.
Aidha alihitaji kufahamu mazao yaliyopangwa kulimwa katika eneo la mradi ambapo Mtaalamu wa Kilimo kutoka wizara ya Kilimo alibainisha kuwa mazao yatakayo limwa katika eneo la mradi ni pamoja na Soya,Mtama,Alizeti pamoja na Mahindi.
Awali akimkaribisha na kutoa ufafanuzi kuhusu Mradi huo, Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, Raymond Mndolwa amesema mradi unaukubwa wa julma ya Hekari 11,000 na umekusudiwa kuleta manufaa ya moja kwa moja kwa Halmashauri ya Chamwino na vijiji vyake.
Kupitia ujenzi wa nyumba za vijana, uwekaji wa miundo mbinu katika eneo la hekari 1000 za Kijiji pamoja na uandaaji wa zaidi ya hekari 400 katika eneo la mradi wa umwagiliaji wa vijana, ambapo eneo lote linawekewa Miundo Mbinu ya Umwagiliaji
Kwa mujibu wa Mndolwa, kila kijana mnufaika wa mradi atapewa hekari 10 na kwamba mpaka sasa nyumba 60 za makazi ya vijana zimeshakamilika kwa asilimia 50.
Mndolwa pia ameongeza Tume imepewa jukumu la kuandaa maeneo ya Michezo, maghala na huduma nyingine za jamii na Kila kijana atapewa hekari kumi na kwamba kuna uchimbaji wa visima 11 ambapo visima 7 vimesha chimbwa na kwamba kutakuwepo pia na ujenzi wa jengo la utoaji huduma za kilimo(Farm House) katika eneo la mradi.
Amebainisha eneo la mradi lina maji mengi ya mvua lakini Tume imejipanga kutumia vyanzo vingine vya maji kupitia uchimbaji wa visima Pamoja na ujenzi wa bara bara zitakazo weza kupitika kipindi chote cha mwaka.
Wakati huo huo Naibu Waziri wa Kilimo David Silinde, amasema Wizara imeelekeza Halmashauri zote nchini kutenga maeneo yatakayo tumika kwa ajili ya ujenzi wa miradi ya vijana na Wizara itafanya kazi ya ujenzi wa miundombbinu ya umwagiliaji na katika eneo la Mradi wa Shamba La Pamoja la Mama Samia, serikali imetenga hekari 1000 kwa ajili ya mradi wa umwagiliaji wa Kijiji na kwamba Halmashauri ya Chamwino pia imetengewa eneo la umwagiliaji
Naye Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule ameishukuru Serikali kwa uwekezaji mkubwa unaofanywa ndani ya Mkoa wa Dodoma, ambapo asilimia 72 ya wakazi wake wanategemea kilimo.”Tumewekewa miundo mbinu ya umwagiliaji na sasa tunauhakika wa kupata Lishe bora,ajira zitaongezeka na uchumi wa mkoa utakuwa”
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Chamwino David Lusinde amesema kwa sasa wananchi wa Chamwino wametoka katika kuzungumzia ukame na sasa wanazungumzia habari za maendeleo ya kilimo kupitia umwagiliaji na anaamini kuwa ukame ulikuwa katika fikra za watu.
Pia amesema Ndogowe na Mlazo watakuwa washiriki na siyo watazamaji, na kwamba Wafugaji wa Chamwino pia wapo na wanatambulika katika eneo hilo la mradi

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...