NA WILLIUM PAUL, DODOMA.

VIJANA wa Chama cha Mapinduzi wametakiwa kutengeneza msingi imara katika kuelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa Novemba mwaka huu ili kuhakikisha Chama kinashinda kwa kishindo kwani ndio Dira ya kuelekea uchaguzi mkuu 2025.

Kauli hiyo imetolewa na Afisa Mwandamizi UVCCM kutoka makao makuu, Kajoro Vyohoroka wakati alipokuwa akitoa semina ya kuelekea uchaguzi kwa viongozi wa Umoja wa Vijana kutoka kata 14 za Jimbo la Same mashariki wilayani Same iliyoandaliwa na Mbunge wa Jimbo hilo, Anne Kilango Malecela katika ukumbi wa Pius Msekwa Bungeni jijini Dodoma.

Alisema kuwa, Chama kikifanya vizuri katika uchaguzi wa Serikali za mitaa itatoa Dira ya kwenda katika uchaguzi mkuu 2025 na kuwataka kuhakikisha wanajitoa kukitafutia Chama kura za kishindo.

Kiongozi huyo aliwataka pia viongozi hao wa UVCCM kujijengea tabia ya kutembelea makundi ya Vijana na kusikiliza changamoto zinazowakabili pamoja na kuzitafutia ufumbuzi kwa kushirikiana na viongozi waliopo madarakani.

"Vijana kwa sasa tumerudi nyuma katika kuwasemea viongozi wetu ambao ni Madawani na Wabunge sasa ifike mahali tuachane na tabia ya kupigana shoti kwa maneno ya uongo bali tuseme mambo mazuri yaliyofanywa na viongozi waliopo madarakani" Alisema Vyohoroka.

Aidha amewataka viongozi hao kukishauri Chama wagombea wanaokubalika na jamii na sio wagombea wa mfukoni ili iwe rahisi kwenda kuwauza kwa wananchi.

Naye Afisa Mwandamizi kutoka makao makuu ya CCM, Frank Uhahula aliwataka viongozi hao kwenda kuhamasisha wananchi kujiunga na Chama cha Mapinduzi na Jumuiya zake ili kwenda na mtaji katika uchaguzi.

Uhahula alitumia pia nafasi hiyo kuwataka viongozi hao kuendesha Jumuiya kwa kufuata kanuni na taratibu za Chama pamoja na kukosoana kwa kutumia vikao maalum na sio kuchafuana katika mitandao ya kijamii.

Kwa upande wake, Mbunge Anne Kilango alitumia nafasi hiyo kuwaomba Vijana kuzingatia yale yote yaliyotolewa na wawezeshaji katika semina hiyo ili kuhakikisha wanakwenda kushinda kwa kishindo uchaguzi wa Serikali za mitaa.

Viongozi walioshirika katika semina hiyo ni Wenyeviti, Makatibu na Makatibu hamasa wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi kata 14 za jimbo la Same mashariki ambapo awali walipata fursa ya kushiriki Bungeni na kujionea shughuli za Bunge zinavyoendeshwa.









Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...