Na Mwandishi wetu, Mirerani

Imeelezwa kuwa miaka nane ya uwepo wa viongozi wazalendo wa benki ya NMB imesababisha mabadiliko kwa wachimbaji kupatiwa mikopo tofauti na awali viongozi wa ngazi za juu waliokuwa wakitokea nje ya nchi.

Mkuu wa idara ya biashara wa benki ya NMB makao makuu, Alex Mgeni ameyasema hayo akizungumza na wadau wa madini ya Tanzanite mji mdogo wa Mirerani wilayani Simanjiro mkoani Manyara.

Mgeni amesema mabadiliko ya uongozi kwa wazalendo wa nchi kuaminiwa na kukabidhiwa dhamana ya uongozi badala ya wageni ndiyo kumesababisha mageuzi hayo ya kupata mikopo.

“Viongozi wetu ambao ni wageni hawakuelewa suala hili la kutoa mikopo kwa wachimbaji madini ila baada ya viongozi wazalendo kupewa nafasi wakatimiza hilo,” amesema Mgeni.

Amesema wametoa mikopo ya vifaa vya kazi kwa wachimbaji wa madini na riba zao huwa ndogo hivyo waliopo kwenye sekta hiyo wachangamkie fursa hiyo ya mikopo NMB.

Amesema hata suala la ukwasi wa benki hiyo limezidi kuwa juu kwani awali walikuwa wanamiliki mali zenye thamani ya Sh3.8 bilioni ila hivi sasa baada ya uongozi mpya imefikia Sh13 bilioni.

Mwenyekiti wa chama cha mabroka Tanzania, Jeremia Simon Kituyo amewataka wanachama wake kujisajili kwenye vyama vyao mikoa yao ili watambulike na kupata mikopo kwa taasisi za fedha.

“Itakuwa vyema mkijisajili na kuwa wanachama wa mikoa yenu ili tuwatambue na benki ya NMB na taasisi nyingine za fedhe ziweze kuwapatia mikopo,” amesema Kituyo.

Ofisa mikopo wa benki ya NMB Tawi la Mirerani, Emmanuel Nyanganyi amesema mabroka 25 wa madini ya Tanzanite, wamewapatia mkopo wa Sh300 milioni.

Makamu Mwenyekiti wa chama cha wachimbaji madini mkoa wa Manyara, (MAREMA) Money Yusuph amesema wachimbaji wanapaswa kuanzisha na kuchangia mfuko wa dhamana.

Money amesema endapo wachimbaji milioni 1 wenye leseni nchini wakichangia shilingi elfu 20 kila mwezi kwa miaka miwili watakusanya 500,000 kila mmoja sawa na shilingi bilioni 5 na kufungua akaunti benki ya NMB.

“Kupitia fedha hiyo shilingi bilioni 5 wachimbaji madini wataweza kujikopesha zana za milipuko na gharama nyingine za uchimbaji bila kuuza nyumba au mashamba yao,” amesema.

Mchimbaji wa madini ya Tanzanite Zephania Joseph ameipongeza benki ya NMB kwani imekuja na mtazamo chanya wa kutoa mikopo kwa wachimbaji kwani awali ilikuwa vigumu.

Mkuu wa kitengo cha biashara wa Benki ya NMB makao makuu, Alex Mgeni (kushoto) akitoa elimu ya mikopo kwa wadau wa madini ya Tanzanite wa mji mdogo wa Mirerani wilayani Simanjiro mkoani Manyara.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...