Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule (wa kwanza kulia), akimsikiliza Bw. Denis Sichalwe (wa kwanza kushoto), kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi akielezea juu ya malisho ya mifugo, uzalishaji wa mbegu na upandikizaji wa mimba kwa ng'ombe jike kwa njia ya chupa (uhimilishaji), katika Maonesho ya Kilimo ya Kimataifa (Nane Nane) 2024 yanayofanyika Kitaifa Mkoani Dodoma

.....

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule amewaasa wataalamu wa sekta za mifugo na uvuvi kupeleka na kufundisha teknolojia za sekta hizo vijijini ili kuwapa wafugaji elimu ya kutosha kuhusu ufugaji wa kisasa kwa lengo la kuleta tija.

Akizungumza, leo Agosti 4, 2024 Mkoani Dodoma alipotembelea kwenye Maonesho ya Kilimo ya Kimataifa (Nane Nane) 2024 yanayofanyika Kitaifa mkoani humo, Mhe. Senyamule amesema wataalamu wahakikishe teknolojia za kisasa zinawafikia wadau wote wa mifugo na uvuvi, hususan maeneo ya vijijini.

"Wataalamu wachukue hatua ya kwenda kwenye makundi ya wafugaji ili kwenda kuwaelimisha kuhusu teknolojia mpya ya ufugaji na kuhakikisha inawafikia" amesema Mhe. Senyamule

Aidha, alisema Serikali ya Awamu ya Sita ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mheshimiwa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, imefanya mapinduzi makubwa sana katika sekta za mifugo na uvuvi kwani ameshuhudia teknolojia mbalimbali na nzuri katika mabanda ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi.

Mhe. Senyamule alisema sekta binafsi pia zimepokea mabadiliko hayo ya kiteknolojia, hususan upande wa vijana wa Jenga Kesho iliyo Bora (BBT) ambao wanatumia teknolojia hizi kama ufugaji wa samaki kwa njia ya vizimba.

Pia, ametoa wito kwa wadau wote wa mifugo na uvuvi kutumia fursa hii ya maonesho haya ya Nane Nane ili kuweza kujifunza na kupata ufahamu juu ya teknolojia za kisasa za mifugo na uvuvi.

*Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule (wa tatu kulia), akizungumza na watendaji wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi kutoka Idara ya Nyanda za Malisho (DGLF), ni katika Maonesho ya Kilimo ya Kimataifa (Nane Nane) 2024 yanayofanyika Kitaifa Mkoani Dodoma.

*Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule (wa kwanza kulia), akimsikiliza Bw. Denis Sichalwe (wa kwanza kushoto), kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi akielezea juu ya malisho ya mifugo, uzalishaji wa mbegu na upandikizaji wa mimba kwa ng'ombe jike kwa njia ya chupa (uhimilishaji), katika Maonesho ya Kilimo ya Kimataifa (Nane Nane) 2024 yanayofanyika Kitaifa Mkoani Dodoma.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule (wa kwanza kulia), akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Bidhaa za Ngozi - CHIBASI, Bw. Freddy Kabala (kushoto), akielezea kuhusu ubora wa viatu vinavyotengenezwa kwa ngozi ya mamba, katika Maonesho ya Kilimo ya Kimataifa (Nane Nane) 2024 yanayofanyika Kitaifa Mkoani Dodoma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...