Waziri Wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za mkoa na Serikali za Mtaa Mohamed Mchengerwa akizungumza na waandishi wa habari mapema leo

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda akimkaribisha Mhe. Mchengerwa huku akimtaja kama kiongozi anayefikika na mwenye umahiri mkubwa katika kuwatumikia wananchi.
Baadhi ya Wa kuu Wa wilaya za mkoa Wa Arusha wakiwa katika Mkutano wWaziri Wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za mkoa na Serikali za Mtaa Mohamed Mchengerwa mapema leo Jijini Arusha




Na. Vero Ignatus, Arusha


Serikali imesema Amri ya Mgawanyo wa Maeneo ya Utawala katika Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya) (Tangazo la Serikali Na. 796 la mwaka 2024) ambalo imetolewa kwa mujibu wa kifungu cha 30 cha Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya), Sura ya 287.


Akizungumza na waandishi Wa Hanari Jijini Arusha Waziri Wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za mkoa na Serikali za Mtaa Mohamed Mchengerwa amesema kuwa Notisi ya Mgawanyo wa Maeneo ya Utawala katika Serikali za Mitaa (Mamlaka za Miji) (Tangazo la Serikali Na. 797 la mwaka 2024) imetolewa kwa mujibu wa vifungu vya 16(1) na 18(1) vya Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Miji), Sura ya 288.


Mchengerwa ameainisha maeneo

Aidha, napenda kueleza kuwa Amri na Notisi hizi ndizo ambazo zimeainisha mitaa, vitongoji, na vijiji vitakavyoshiriki katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika tarehe 27 Novemba 2024. Uchaguzi huu ni muhimu kwa ustawi wa demokrasia yetu na maendeleo ya Serikali za Mitaa.
Katika amri na notisi hizi, jumla ya maeneo yafuatayo yameainishwa: ni pamoja na Jumps ya bikini 12,333,Mitaa 4,269, Vitongoji 64,274

Aidha amesisitiza kuwa Matangazo haya yanajumuisha maeneo yaliyokuwa yamefutwa awali kwa mujibu wa Tangazo la Serikali Na. 673 na 674, ambayo yalihusisha pia Tarafa ya Ngorongoro. Lengo la hatua hii ni kuhakikisha kuwa maeneo haya yanapata uwakilishi mzuri wa kiutawala, pamoja na huduma za kijamii na kiuchumi zinazowiana na mahitaji ya wananchi wake.

Mchakato huu ni fursa kwa wananchi kushiriki moja kwa moja katika kuamua mustakabali wa maendeleo ya maeneo yao. Uongozi imara katika ngazi ya mitaa, vitongoji na vijiji unahitajika ili kuendeleza juhudi za Serikali za kujileta maendeleo endelevu.

"Orodha ya Wapiga Kura itakapofika Oktoba 11 hadi 20, ambayo itatumika siku ya uchaguzi tarehe 27. Pili, tunawahimiza wale wenye nia ya kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika Serikali za Mitaa kuchukua hatua za mapema za kujiandaa na kushiriki kikamilifu".Alisema

Akitoa salamu za mkoa Mhe. Paul Christian Makonda amemuahidi Mhe. Mchengerwa kusimamia maelekezo yote aliyoyatoa kuhusu uchaguzi ujao wa serikali za mitaa, ikiwemo kuhakikisha kuwa wananchi wa Tarafa ya Ngorongoro wanashiriki uchaguzi huo kikamilifu kulingana na sheria na miongozo iliyopo.

Vilevile Makonda alisema Mkoa Wa Arusha Paul Christian mkoa huo upo salama, watu wanaojitambua na wanatafuta pesa kwa jasho Lao wakiwemo wafanyabiashara mbalimbali ikiwemo Madini, wakulima, wafugaji

Kwa upande wake Mwenyekiti Wa Halmashauri ya Ngorongoro Mmarekani Bayo amesema wameipokea Amri hiyo kwa furaha wao kama Tarafa ya Ngorongoro kwamba na wao wameingia kwenye mgawanyo huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...