Na Chalila Kibuda,Michuzi TV


Chuo cha  Ufundi Stadi (VET) Furahika kinatarajia kufanya mahafali Septemba 28 mwaka huu katika viwanja vya St.John Buguruni Malapa jijini Dar es Salaam huku mgeni rasmi wa Mahafali hayo Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Dar es Salaam.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam Mkuu wa Chuo hicho Dkt.David Msuya amesema  kuwa wahitimu hao ni wale wanafunzi Elimu bure katika kuunga jitihada za Serikali ya Awamu ya Sita ya Dkt.Samia Suluhu Hassan ya kuwaandaa vijana kwenye ujuzi ili waweze kuzalisha.

Amesema kuwa katika jitihada hizo fani ya utalii asilimia 75 wameweza  kuajirika kutokana na kuwaandaa vijana kwa weledi.

Amesema wanawapokea vijana kuanzia darasa la saba imekuwa ni faraja  kutokana  na kupata  urahisi wa  kuajirika huku akisifu sekta binafsi ya wamiliki wa hoteli kutoa kipaumbele kwa vijana hao.

Amesema kuwa Chuo hicho wanatarajia kwenda kutoa elimu ya ukatili kwa vijana Zanzibar.

Amesema kuwa mfumo walioanza nao wa elimu ya ukatili wa kijinsia ni kwenda katika mashina ya wajumbe ambapo huko ndio tatizo linakoanzia.

Amesema kuwa vijana wengi hawashiriki katika elimu mbalimbali kutokana na mazingira kuwa elimu hizo zinaanzia ngazi ya Kata hadi Taifa na kuacha kiini cha tatizo kwenye mashina.

Hata hivyo amesema kuwa wanawaomba wadau kujitokeza katika kutoa misaada mbalimbali ikiwemo magari hata kama mabovu watayatengeneza.

Amesema Taasisi hiyo wanafunzi wanatoa sehemu ya usajili wa mitihani yao kwa kiasi cha Sh.50,000 ambapo fedha hiyo chuo haipati kabisa.

Dkt.Msuya amesema kuwa kazi ya Serikali inafanya vitu vingi hivyo lazima tujenge mazingira kama wadau kutoa mchango wetu.
Mkuu wa Chuo cha Ufundi  Stadi (VET) Furahika Dkt.David Msuya akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na Mahafali ya chuo hicho na mikakati mbalimbali waliojiwekea katika utoaji wa Elimu Bure kwa vijana ,jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...