Na. Abel Paul Chicago Marekani.
Askari wa kike kutoka nchini Tanzania wakiwa katika Jiji la Chicago Nchini Marekani wametumia fursa ya Mafunzo yaliyofanyika nchini humo kutangaza Utalii na vivutio vya vilivyopo nchini ikiwa ni kuunga mkono Juhudi za mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama nchini Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan katika Kuutangaza utalii.
Akiongea mara baada ya mafunzo hayo kamishna wa Polisi Utawala na Menejimenti ya rasilimali watu wa Jeshi la Polisi kutoka Nchini Tanzannia CP Suzan Kaganda amesema kuwa wamehitimisha mafunzo nchini humo huku akiweka wazi kuwa wametumia fursa hiyo ya maelefu ya askari na wasimamizi wa sheria kuwaeleza vivutio vilivyopo nchini Tanzania.
CP Kaganda ameongeza kuwa waliamua kuvaa mavazi ambayo yanaakisi utalii na vivutia vya utalii lengo likiwa kuendelea kutangaza Utalii na vivutio vilivypo nchini Tanzania ambapo amebainisha kuwa askari kutoka nchini Tanzania kwa umoja wao wamejitahidi kuwafikia washiriki na kuwatangazia Utalii na vivutio vilivyopo nchini Tanzania.
Kwa upande wake Mrakibu mwandamizi wa Polisi SSP Geogina Matagi ambaye ni Mkuu wa Polisi Wilaya ya Arusha Nchini Tanzania yeye akajinasibu kutokana na kutangaza utalii nchini marekani Mkoa wake ambao ni kitovu cha Utalii Nchini Tanzania utakavyonufaika na ujio wa wageni wengi ambao wamepata kusikia sifa Tanzania katika mafunzo nchini Marekani.
Nae Naibu Kamishna wa Uhamiaji kutoka nchini Tanzania DCI Bahati Mwaifuge mbali nakutangaza vivutio vya utalii amesema kuwa wamewaambia endapo watafika Nchini Tanzania watapatakuona vivuti vingi ikiwa ni Pamoja na madini ya Tanzanite yanayopatikana Tanzania peke.
Mshiriki kutoka Mkutano huo yeye akaeleza namna ya upendo ulioonyesha na washiriki wa Tanzania kitendo kilichomvutia na kumpa taswira nzuri ya Afrika na Tanzania huku akiweka wazi mpango wake wa kutembelea Tanzania ilikujionea vivutio vilivyopo nchini Tanzania.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...