Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Dayosisi ya Karagwe Dkt. Benson Bagonza ameutaka Mwenge wa Uhuru 2024 kuwamulika Maadui wa Maendeleo waliomo Nchini ikiwa ni katika Dhana ya kuwafichua Maadui wa Maendeleo ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Askofu Bagonza ametoa wito huo wakati alipopata nafasi ya Kutoa salaam zake kwa Wananchi wa Wilaya ya Karagwe Eneo la Kishao, wakati wa Tukio la Uzinduzi wa Mradi wa Barabara yenye ya lami Kishao - Lukajange yenye Urefu wa Km 0.7 yenye thamani ya Shilingi Milioni 358.08 inayotekelezwa chini ya Tarura.

Katika salaam hizo Askofu Bagonza amewakumbusha Wananchi historia na Dhana ya Mwenge wa Uhuru Toka ulipopandishwa Juu ya Mlima Kilimanjaro na Brigedia Alexander Donald Nyirenda Mwaka 1961, ilikuwa ni kuwamulika Maadui waliopo Nje na Ndani ya mipaka ya Nchi yetu, lakini kwa Sasa Maadui wa namna hiyo hawapo tena, Bali wameibuka Maadui wa ndani ya Nchi Wapinga Miradi ya Maendeleo, Hivyo Mwenge wa Uhuru uendelee kuwamulika na kuwafunua Ili Wananchi waendelee kunufaika na Miradi kama hii ya Maendeleo inayoletwa na Serikali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...