Yuko Pia Mwanae Na Wenzake Wawili
Na Karama Kenyunko Michuzi Tv
BIBI, Felista Mwanri (70), na mtoto wake, Richard Mwanri (47) wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam wakikabiliwa na tuhuma za kusafirisha zaidi ya tani moja ya dawa za kulevya aina ya bangi aina ya skanka
bibi Felista na mtoto wake wanashtakiwa pamoja na Athuman Mohamed maarufu kwa jila la Makame (58) mkazi wa Tanga, Juma Chappa (36) mkazi wa Kiwalani na Omary Mohamed (32) ambae ni dereva anayeishi Buza, Dar es Salaam.
Katika hati ya mashtaka iliyosomwa mahakamani hapo na wakili wa Serikali Eric Davis leo Septemba 10,2024 mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Godfrey Mhini imedai washtakiwa wanatuhumiwa kwa shtaka moja la kusafirisha dawa za kulevya kinyume na sheria.
Imedaiwa, Agosti 28,2024 washtakiwa wakiwa eneo la Tairo Luguruni barabara ya Kwembe ndani ya Wilaya ya Ubungo ǰijini Dar es Salaam walikutwa walisafirisha kilogramu 1815 za dawa za kulevya aina ya bangi.
Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika na washtakiwa hawakuruhusiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo kwa kuwa kesi inayowakabili ni ya uhujumu uchumi. Wote wamerudishwa mahabusu
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Septemba 24,2024 kwa ajili ya kutajwa na kuangalia hatua ya upelelezi ilipofikia.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...