Linda Akyoo - Moshi

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kilimanjaro Ndugu Patrick Boisafi ameambatana na wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Mkoa wametembelea mradi wa  Maabara ya kisasa ya kupima ubora wa Maji ambao umetekelezwa na wataalamu wa ndani kutoka Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Moshi (MUWSA) na kuridhishwa na utekelezaji wake.

Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa mradi huo mbele ya Kamati hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Moshi (MUWSA) Mhandisi Kija Limbe amesema kiasi cha Shilingi Milion 81,859,500 zimetumika kwa ajili ya ujenzi pamoja na ununuzi wa baadhi ya vifaa vya Maabara hiyo fedha zilizotoka mapato ya ndani ya Mamlaka hiyo na mradi huo umekamilika kwa asilimia 100.

Aidha, Kamati hiyo imeweka wazi kuridhishwa na utekelezaji wa mradi huo ambao thamani ya fedha zilizotumika zinaonekana.

Mradi huo unalenga kuhudumia zaidi ya wananchi 592,132 wanaohudumiwa na Mamlaka kwa eneo la Manispaa pamoja na Halmashauri ya Moshi.

Ujenzi wa maabara hiyo ya kisasa  unalenga kuendelea kuwahakikishia wananchi usalama wa maji wanayokunywa kutoka bombani.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...