Na Munir Shemweta, WANMM


Changamoto ya usafiri inayowakabili watumishi wa wizara ya ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi sasa inaenda kupungua kufuatia wizara hiyo kukabidhiwa basi jipya aina ya TATA lenye thamani ya shilingi milioni 170.

Makabidhiano ya gari hiyo yamefanyika jijini Dodoma leo Septemba 19, 2024 baina ya Meneja Uendeshaji wa Kampuni ya TATA Africa Holdings (Tanzania) Limited Bi. Muareen Kiputa na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Seushi Mbuli kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo na kuhudhuriwa na baadhi ya watumishi wa wizara Makao Makuu.

Kupatikana kwa basi hilo kuinaifanya Wizara ya Ardhi kuwa na mabasi matatu yatakayopunguza changamoto ya usafiri kwa watumishi wa wizara hiyo hususan pale wanapokwenda na kurudi ofisini sambamba na shughuli nyingine za wizara nje ya makao makuu ya wizara.

Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara ya Ardhi Bw. Seushi Mbuli amesema, kupatikana kwa basi hilo kutapunguza kwa kiasi kikubwa changamoto ya usafiri kwa watumishi wa wizara hiyo hasa pale wanapokweda na kurudi maofisini.

Ameongeza kuwa, kununuliwa kwa basi hilo ni jitihada za Wizara ya Ardhi kuhakikisha watumishi wake hawapati shida ya usafiri wakati wa kwenda kutekeleza majukumu yao katika maeneo mbalimbali.


‘’Nina imani kubwa sasa changamoto ya usafiri kwa watumishi wetu itapungua sana kutokana na ujio wa basi hili’’. alisema MbuliMkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bw. Seushi Mbuli akikabidhiwa nyaraka za umiliki wa basi aina ya TATA kutoka kwa Meneja Uendeshaji wa Kampuni ya TATA Africa Holdings (Tanzania) Limited Bi. Muareen Kiputa leo tarehe 19 Sept 2024. Katikati ni Mkurugenzi Msaidizi Utawala Bw. Simbani Liganga Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bw. Seushi Mbuli (Wa tatu kulia) na Meneja Uendeshaji wa Kampuni ya TATA Africa Holdings (Tanzania) Limited Bi. Muareen Kiputa (wa pili kulia)) wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa Wizara ya Ardhi Makao makuu mara baada ya makabidhiano ya basi aina ya TATA lenye thamani ya milioni 170.




Muonekano wa basi aina ya TATA lililokabidhiwa kwa wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Sept 19, 2024 jijini Dodoma.Baadhi ya Watumishi wa Wizara ya Ardhi ndani ya basi jipya aina ya TATA (PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI)



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...