Na. Vero Iganatus
Mkuu Wa Wilaya Ya Karatu Mhe. Dadi Kolimba awataka wanchi wa wilaya ya Karatu kutokeza kujiandikisha katika daftari la wakazi la wapiga kura zoezi ambalo linatarajiwa kuanza tarehe 11/10/2024 hadi tarehe 20/10/2024.
Mhe.Kolimba amesema zoezi hilo ni muhimu sana kwa wakazi wa wilaya ya Karatu kwani litawapa fursa ya kuwachagua viongozi katika uchaguzi utakaofanyika Novemba 27 mwaka 2024 kwa maendeleo yao na wilaya kwa ujumla.
Aidha, Mhe. Kolimba amefafanua sifa kuu wananchi wanaopaswa kuwanazo ili kushiriki zoezi la kujiandikisha ikiwemo. kuwa mtanzania halali, mkazi wa eneno husika, umri usiopungua miaka 18 na pia kuwa na akili timamu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...