MKUU wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogogolo, amesema serikali imejipanga kikamilifu kuanza ujenzi wa barabara katika Kata za Kivule, Mzinga, Kipunguni na Kitunda,kupitia Mradi wa Uboreshaji wa Miundombinu ya Jiji la Dar es Salaam (DMDP) .
Ameyasema hayo Dar es Salaam,akiwa katika ziara ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi wa kata hizo.
Amesema tayari Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, imetia saini mkataba wa utekelezaji wa mradi huo na kata hizo zitanufaika.
“ Awali tulipanga kujenga barabara zenye jumla ya urefu wa kilometa 46 lakini tumeongeza idadi ya barabara hivyo jumla ni kilometa 57 ndiyo zitakazo jengwa,” alisema Mpogogolo.
Ametaja miongoni mwa baraba zitakazo jengwa ni Kitunda- Kivule hadi Msomgola yenye urefu wa Kilmetea 9.95, Kivule -Majohe Kilomita2.79.
Amesema kwa upande wa Halmashauri ya Jiju la Dar es Salaam, imetenga sh. bilioni 10 kujenga jumla ya kilomete 10 na tayari mikataba imesainiwa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...