BENKI ya Equity imeingia makubaliano na kampuni ya Bakhresa yenye lengo la kutoa mikopo kwa wafanyabiashara wa unga, ambapo mfanyabiashara atakuwa na uwezo wa kukopa fedha kwa ajili ya kupata bidhaa hiyo mpaka zaidi ya Shilingi Milioni 300.
Akizungumza leo Septemba 26,2024 Jijini Dar es Salaam katika hafla hiyo, Mkurugenzi wa Biashara wa benki ya Equity Leah Ayoub amesema lengo ni kuhakikisha wafanyabiashara wanakuza mitaji ambapo kama benki wanatamani wateja hao wakope zaidi ya Sh Milioni 300.
“Tumeingia makubaliano kati ya benki ya Equity na kampuni ya Bakhresa yenye lengo la kutoa mikopo kwa wafanyabiashara wa unga,mfanyabiashara atakuwa na iwezo wakukopa fedha kwa ajili ya kuoata bidhaa hiyo mpaka zaidi ya Shilingi Milioni 300,”amesema.
Amesema mkopo huo hautakuwa na riba isipokuwa mteja atalipa kamisheni yakuanzia asilimia 0.5 mpaka 1.5 ambapo mkopaji atapaswa kulipa fedha hizo kuanzia siku saba hadi 30.
“Hii ni fursa ya kukuza mtaji wako kwa haraka,tumeamua kujitoa kwa wajasiriamali na kuwawezesha wapate huduma kwa urahisi bila vikwazo vingi ambapo mteja hata kama hana akaunto ya Equity ana uwezo wakuifungua kiganjanjani mwake akapata mkopo,”amesema Leah.
Naye Mkurugenzi wa Uhusiano wa kampuni Bakhresa Group Hussein Sufiani amesema makubaliano hayo yatamsaidia mteja ambapo badala kuhangaika kutafuta mfadhili au mdhamini wa kumpatia fedha anaweza kwenda benki au kutumia mtandao kupata huduma.
“Hii nayo ni kidigitali, utapata huduma hiyo kwa mfumo wa sms (ujumbe mfupi), sio lazima uende benki kufanya transfer (kuhamisha) inafanyika moja kwa moja ukishafanya oda yako, kadri unavyozidi kukopa kiwango kinakua,”amesema Sufiani.
Amesema huduma hiyo itawasaidia zaidi wateja wao hasa wadogo hivyo amewahimiza kuchangamkia fursa hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...