LEO hii Jumamosi ya Septemba 14 2024, Kampuni ya ubashiri Tanzania Meridianbet, imetoa msaada wa vifaa vya hospitali kwa Hospitali ya Kijitonyama, ikiwa ni sehemu ya jitihada zake za kusaidia jamii na kuboresha huduma za afya nchini.


Msaada huo ambao Meridianbet wameamua kutoa ni mashuka pekee ambayo haya yatawasaidi kwenye kutandika vitanda vya wagonjwa katika hospitali hiyo, vifaa vya usafi, pamoja na vifaa vingine muhimu vya matumizi ya hospitalini. Hatua hii inakuja katika wakati muafaka ambapo hospitali nyingi nchini zinakabiliwa na changamoto ya upungufu wa vifaa vya kutosha vya matibabu na hata ukienda vinakuwa havikidhi mahitaji.

Akizungumza wakati wa tukio hilo la kukabidhi vifaa hivyo, Mhariri wa Meridianbet, Bi. Nancy Ingram alisema:
"Tunatambua umuhimu wa sekta ya afya katika maendeleo ya Taifa, na tunajivunia kuchangia katika kuboresha mazingira ya utoaji huduma za afya kwa wananchi. Meridianbet inajikita katika kujenga uhusiano mzuri na jamii kwa kutoa misaada inayosaidia kuinua ustawi wa wananchi, hasa katika nyanja muhimu kama afya."

Aidha, wauguzi wa afya wa hospitali hiyo ya Kijitonyama baada ya kufikiwa na kampuni hiyo ya ubashiri aliwashukuru kwa msaada huo, akisema kuwa utaboresha kwa kiasi kikubwa huduma zinazotolewa hospitalini hapo na kuzingatia usafi kwa wagonjwa wengi.

Msaada huo ni sehemu ya mpango mpana wa kijamii wa Meridianbet unaolenga kuchangia katika maendeleo ya sekta mbalimbali ikiwemo elimu, michezo, na afya. Kampuni hii inaendelea kuwa mstari wa mbele katika kusaidia jamii kwa kuwekeza rasilimali zake kusaidia wale wanaohitaji zaidi.

Kama bado hujajisajili na Meridianbet muda ndio huu sasa, ingia na usuke jamvi lako la leo kwani pesa ni nje nje Jumamosi ya leo, Liverpool, PSG, Real Madrid, Bayern wote wapo uwanjani kukupa pesa. Jisajili hapa.

Meridianbet imekuwa sasa ni kawaida yao kurejesha kwenye jamii kwani jamii ina mahitaji mengi na inahitaji kusaidiwa kwa kile ambacho kinawezekana kwa wakati huo, hivyo ndio maana kampuni hiyo iliamua kuwafikia Kijitonyama.

Meridianbet ni kampuni inayoongoza katika michezo ya kubashiri nchini Tanzania, ikiwa na uzoefu wa miaka mingi katika tasnia hii. Pamoja na huduma zake za michezo ya mtandaoni, pia inatoa michezo ya kasino ya mtandaoni kama vile, Aviator, Poker, Roulette, Sloti na mengine kibao ambayo unaweza kucheza na kupiga pesa.

Meridianbet inajivunia kuwa sehemu ya jamii kwa kuchangia katika shughuli mbalimbali za kijamii na kusaidia kuboresha maisha ya Watanzania.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...