Na Nasra Ismail, Geita


Maadhimisho ya kitaifa ya maulid ya kuzaliwa kwa mtume Muhammad yanatarajiwa kufanyika usiku wa septemba 15/16 katika viwanja vya CCM kalangalala mkoani Geita.

Akitoa taarifa hiyo sheikh mkuu wa mkoa alhaji Yusuph Kabaju mbele ya waandisishi wa habari alisema kuwa maulid hiyo inatarajiwa kuwa ya kipekee ambayo itatambulika kama Maulid ya dhahabu ambayo itakutanisha makundi mbalimbali ya viongozi wa kidini toka nchi nzima.

Aidha sheikh Kabaju aliongeza kuwa maulid hii itatanguliwa na wiki ya maulid ambayo itaanza September 9.

"Hii ni kwa sababu mkoa wetu wa Geita kama mnavyofahamu ni mkoa wenye madini ya dhahabu, tunataka watu waje wajionee na kushuhudia fadhila za mwenyezi Mungu," amesema.

"Mgeni rasmi katika Maulidi ya kitaifa anatarajiwa kuwa mheshimiwa Mufti na Shehe mkuu wa Tanzania na mgeni rasmi katika baraza kuu la Maulid kitaifa anatarajiwa kuwa Rais Dk Samia Suluhu Hassan," amesema.

Amesema maadhimisho ya Maulid yataambatana na semina ya maalum kwa makundi tofauti itakayojumuisha masuala ya ukatili wa kijinsia chini ya wazungumzaji mbalimbali kutoka makao makuu.


Katibu Bakwata mkoa wa Geita, Abbas Mtunguj ya amesema Mufiti wa Tanzania, Shehe Abubakar Zubeir bin Ally anatarajiwa kuwasili Geita kupitia uwanja wa ndege Chato siku ya Septemba 12.

Amesema baada ya kuwasili Mufiti atazuru kaburi la Hayati Dk John Magufuli na kasha kwenda kuzindua jengo la msikiti uliojengwa na Naibu Waziri Mkuu Dk Dotto Biteko Ushirombo wilayani Bukombe.

"Tutakuwa na makongamano yatakayohusisha makundi matatu, kundi la kwanza litakuwa ni maimamu na mashehe, kundi la pili litakuwa ni kongamano la vijana, kongamano la tatu litakuwa ni la kina mama," amesema.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...