NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, John Mongella, alikabidhiwa taarifa ya utekelezaji wa mradi wa upanuzi wa skimu ya maji kutoka kijiji cha Nyankende hadi kijiji cha Mwadui, Halmashauri ya Ushetu, mkoani Shinyanga, tarehe 8 Septemba 2024.
Meneja wa RUWASA Wilaya ya Kahama, Mhandisi Maduhu Magili, alieleza kuwa mradi huo unatarajiwa kukamilika ndani ya mwezi huu wa Septemba 2024. Lengo kuu ni kutatua tatizo la upatikanaji wa maji safi na salama kwa wakazi wa kijiji cha Mwadui, sambamba na kuunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya sita za kumtua mama ndoo kichwani.
Chanzo cha maji kwa mradi huo ni kisima kirefu kilichopo kijiji cha Nyankende, chenye uwezo wa kuzalisha lita 14,000 kwa saa. Mradi huu, ukiwa umekamilika kwa asilimia 85, utahudumia takriban wakazi 2,058 wa kijiji cha Mwadui na unatarajiwa kugharimu zaidi ya shilingi milioni 300.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...