Washiriki kutoka Nchi 12 za ukanda wa Mashariki na kushiriki Mafunzo ya Wataalam wanaohusika na Mambo ya Nishati wakiwa katika picha ya pamoja
Mtaalam Sourian Hachad akiendelea kutoa ufafanuzi namna ya kutumia vyanzo vingine kwaajili ya kuzalisha umeme


Wa kwanza kushoto ni Naibu katibu mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Tenkolojia Prof. Daniel Mushi akibadilishana mawazo na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TAEC Dkt. Justine Ngaile katika mafunzo ya wataalam wanaohusika na Mambo ya Nishati Jijini Arusha





Na. Vero Ignatus,Arusha


Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia imesema itaendelea kuwajenga uwezo vijana wengi kupitia TAEC ili waweze kupata weledi nzuri zaidi wa kutengeneza umeme kutoka kwenye madini ya nyuklia ili uweze kufika kila mahali.

Naibu katibu mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Tenkolojia Prof. Daniel Mushi amesema hayo mapema leo 10/9/2024 wakati akifungua warsha ya Mafunzo ya Wataalam wanaohusika na Mambo ya Nishati kutoka nchi 12 za ukanda wa Mashariki ya Afrika lengo likiwa ni kujipanga kwa pamoja namna ya kufanya nchi hizo kuwa na umeme wa uhakika

"Leo hii tumekutana hapa chini ya mwavuli Taasisi inayoitwa International Atomic Energy ambayo inasimamia Mambo ya mionzi duniani kote, natunajua kuna uwezekano wa kupata umeme kutoka kwenye madini haya yanayozalisha nyuklia kwa hiyo tu nataka tuweze kuona namna ambavyo nchi set up za ki Afrika zikazalisha umeme kupitia viini vya vyuklia"alisema.

Prof. Mushi amesema Miaka mingi walitegemea umeme unaozalishwa kutoka kwenye maji, hivyo wanaangalia kutokana na mabadiliko ya tabianchi chanzo hicho hakitoweza kuwa tegemezi tena bali nchi zote zilizokutana kwenye Mafunzo hayo kwa pamoja wanahitaji kufikiria vyanzo mbadala

"Tunafahamu tumepiga hatua kama Nchi umeme unapatikana kwa kiasi kikubwa lakini tunahitaji kuhakikisha kwamba nchi nzima imepata umeme, kwani nchi yetu ni kubwa Ila tunakiri kwamba jitihada kubwa zimefanyika na umefika mahali pengi ili tujinitosheleza tuweze kuwauzia na wenzetu na kupamata faida kwenye vyanzo ambavyo Mwenyezi Mungu ametupatia".Alisema Prof. Mushi

Aidha amesema kuwa tayari Nchi ya Afrika ya Kusini wameshapiga hatua hivyo wanataka kuona nchi hizo za ukanda wa mashariki namna gani wanaweza kutimia chanzo hicho cha vyuklia kupata umeme toshelevu

"Tunafahamu tunayo madini ambayo yanaweza kutumika katika kuzalisha umeme wa nyuklia kwa mfano Uranium ambapo hapa nchini ipo kubwa kwa hiyo wakati umefika sasa tone nna ya kutumia madini hayo kuzalisha umeme wa uhakika

Prof. Mushi amesema maendeleo ya viwanda hayawezekani bila ya kuwa na umeme wa kutosha, kwani nchi zote zilizoshiriki katika Mafunzo hayo zinauhaba wa umeme hivyo zinahitaji kupata vyanzo mbadala.

"Tumekuwepo na Taasisi ya Eastern African power pool ambayo inahamasisha kuunganisha gread setup za Taifa ili tuweze kuuziana umeme wa ziada ambao tunao ili mwisho wa siku tujitosheleze kutokana na vyanzo hivi mbalimbali tunavyoweza kuvitumia hapa kwetu tunahitaji kuwa na Nguvu za pamoja ili tuweze Kufiaka mbali zaidi ili tuweze kuchochea maendeleo ya kiuchumi na ya kijamii.

Mtaalam Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomiki Mohamed Bassam Ben Teacher pamoja na kusisitiza kupata vyanzo vya kupata umeme hawawezi kupuuza vyanzo vingine, bado wanasisitiza vyanzo viendelee kutumika

Teacher amesema kuwa Kwa kuwa Afrika bado haina umeme wa kutika Shirika la Kimataifa Nguvu za Atomiki linaendelea kuongeza juhudi za kuhakikisha inapata umeme

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...