WAZIRI wa Katiba na Sheria, Prof. Palamagamba Kabudi,akizungumza na moja wa mteja mara baada ya kuzindua Kituo cha Huduma kwa Mteja ,uzinduzi huo umefanyika katika Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma.
Na Mwandishi Wetu, DODOMA
WIZARA ya Katiba na Sheria imezindua Kituo cha Huduma kwa Mteja huku Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia (Mama Samia Legal Aid Campaign), imetajwa kuleta hamasa kubwa kwa wananchi kuwasilisha malalamiko na hoja za kisheria zinazohitaji ufumbuzi wa haraka.

Akizungumza leo Septemba 5,2024 katika Mji wa Kiserikali Mtumba jijini Dodoma kwenye uzinduzi wa kituo hicho, Waziri wa Katiba na Sheria, Prof. Palamagamba Kabudi, amesema kuwa serikali imeanzisha kituo hicho baada ya kubaini wananchi wamekuwa wakiwasilisha malalamiko mengi kwa njia ya barua na wengine wakitumia gharama kubwa kusafiri kuyapeleka wizarani Dodoma.

Amesema kuwa kupitia kampeni hiyo ambayo hadi sasa imefika mikoa ya Dodoma, Manyara, Singida, Simiyu, Shinyanga, Ruvuma na Njombe imechochea kuanzishwa kwa kituo hicho.
Amesema kituo hicho ni muendelezo wa kampeni hiyo ambayo hivi karibuni itaendelea kwenye mikoa iliyosalia ya Tanzania Bara na Zanzibar.

“Kituo hichi ni utekelezaji wa falsafa ya R nne za Rais Samia Suluhu Hassan ambazo ni Maridhiano, Ustahimilivu, Mabadiliko na Kujenga upya, kupitia falsafa hizi wizara inawezesha utatuzi wa migogor, inatoa elimu na msaada wa kisheria,”amesema Prof.Kabudi.

Amebainisha kuwa serikali iliamua kuanzisha kituo hicho ambapo mwananchi anaweza kuwasilisha hoja yake kupitia namba ya simu 0262160360.
“Hii imesaidia kwa wananchi wasio na uwezo wa kumudu gharama za usafiri kuja kuwasilisha malalamiko yao wizarani, kwasasa wananchi walio maeneo ya mbali sasa wana uwezo kuwasilisha malalamiko yao kwa njia ya simu kwenye kituo hichi na kufanyiwa kazi bila kufika wizarani,”amesema

Ameeleza kuwa takwimu za mwezi Februari hadi Agosti 31, 2024, malalamiko 499 yamesajiliwa na kati ya hayo 410 sawa na asilimia 82 yamefanyiwa kazi kikamilifu na 89 yapo hatua mbalimbali ya kutafutiwa ufumbuzi.

Aidha amesema wananchi wanakabiliwa na kero nyingi na kuanzishwa kwa kituo hicho ni dhamira ya serikali kutumia njia rahisi za kiteknolojia kuwafikia wananchi ili kutatuliwa kero zao kwa wakati.

“Wizara inampango wa kuongeza muda wa kutoa huduma uwe saa 24 na siku saba kwa wiki, niwashukuru wadau wa maendeleo FCDO kwa kufanikisha uwepo wa kituo hichi kwa kushirikiana bega kwa bega na serikali,”amesema.

Hata hivyo ameviomba vyombo vya habari kuendelea kutoa elimu kwa jamii uwepo wa kituo hicho ili wananchi wawasilishe malalamiko yao yafanyiwe kazi.

Awali, Mkurugenzi wa Idara ya Katiba na Ufuatiliaji Haki wa Wizara hiyo,Bi. Jane Lyimo, amesema uwapo wa kituo ni mikakati ya kukabiliana na rushwa kupitia program inatotekelezwa na wizara hiyo inayosimamiwa na Ofisi ya Rais, Ikulu kupitia ufadhili wa serikali ya Uingereza.

Amesema kutokana na umuhimu wa kituo hicho ni muhimu taasisi za serikali kushirikiana na Wizara ili kutatua hoja za kisheria na kurahisisha mchakato wa kumhudumia mwananchi.

WAZIRI wa Katiba na Sheria, Prof. Palamagamba Kabudi,akizungumza wakati wa uzinduzi wa kituo cha Huduma kwa mteja,uzinduo huo umefanyika leo Septemba 5,2024 katika Mji wa Kiserikali Mtumba jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Idara ya Katiba na Ufuatiliaji Haki wa Wizara ya Katiba na Sheria Bi.Jane Lyimo,akizungumza wakati wa uzinduzi wa kituo cha Huduma kwa mteja,uzinduo huo umefanyika leo Septemba 5,2024 katika Mji wa Kiserikali Mtumba jijini Dodoma.

SEHEMU ya washiriki wakimsikiliza Waziri wa Katiba na Sheria, Prof. Palamagamba Kabudi (hayupo pichani),akizungumza wakati wa uzinduzi wa kituo cha Huduma kwa mteja,uzinduo huo umefanyika leo Septemba 5,2024 katika Mji wa Kiserikali Mtumba jijini Dodoma.

WAZIRI wa Katiba na Sheria, Prof. Palamagamba Kabudi,akizungumza na moja wa mteja mara baada ya kuzindua Kituo cha Huduma kwa Mteja ,uzinduzi huo umefanyika katika Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma.

WAZIRI wa Katiba na Sheria, Prof. Palamagamba Kabudi,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuzindua kituo cha Huduma kwa mteja,uzinduo huo umefanyika leo Septemba 5,2024 katika Mji wa Kiserikali Mtumba jijini Dodoma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...