RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk Samia Suluhu Hassan ametoa kiasi cha Million 30 kwa timu Taifa ya wasichana ‘Serengeti Girls’, baada ya kutwaa ubingwa wa Mashindano ya Mpira wa Miguu kwa nchi za Kaskazini mwa Afrika (UNAF U-17) katika mashindano yaliyofanyika nchini Tunisia 2024.

Akikabidhi kitika hicho leo Septemba 11, 2024 Jijini Dar Es Salaa Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amewapongeza wachezaji hao kwa kuiwakilisha vyema Taifa huku akiwataka kujituma na kupambana zaidi ili kujipatia nafasi ya kwenda kucheza soka la kulipwa kwa ajili ya kujenga timu ya taifa imara ya wanawake. 

“Rais Samia amefurahishwa sana na ushindi huo na kutoa zawadi ya mama kwa kutoa kiasi cha milioni 30, kwa kuwakabidhi milioni 10 na kesho kutwa (ijumaa, Agosti 12) tutawamalizia milioni 20 kwa sababu ya changamoto ya mfumo” amesema Mhe. Ndumbaro

Aidha, Mhe. Ndumbaro ameongeza kuwa ni maelekezo ya Rais Samia kuwa, wahakikishe timu zote za Taifa zinafanikiwa kufuzu fainali za AFCON pamoja na Kombe la Dunia.







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...