Naibu waziri wa madini Dkt Steven Kiruswa ametembelea katika ujenzi wa mradi wa kiwanda kidogo cha majaribio ya uchimbaji madini ya Uranium unaozalishwa na kampuni ya uchimbaji madini MANTRA uliopo kijiji cha Likuyu wilaya ya Namtumbo mkoa wa Ruvuma


Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Likuyu wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma amesema wananchi waachane na dhana potofu kwamba uchimbaji wa madini ya Uranium utaenda kuathiri afya za wananchi waliopo karibu na maeneo ya migodi kwani serikali haiwezi kuruhusu wananchi wapate madhara kwa kuhakikisha kabla hawajafanya shughuli za uchimbaji serikali lazima wachunguze na wajiridhishe kua mradi huo hautakua na madhara yeyote kwa jamii ndipo wawaruhusu wawekezaji kufanya shuguli za uchimbaji madini.



Naibu waziri Steven Kiruswa amesema anamshukuru Mheshimiwa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutengeneza mazingira mazuri kwa ajili ya uwekezaji nchini na amewasihi wananchi kutoa ushirikiano kwa wawekezaji na kwenda kua mabalozi wazuri kwa wapotoshaji kwani kupitia fursa hii inaenda kuinua uchumi wa nchi kutokana na madini ya Uranium kua miongoni mwa madini pekee yanayopatikana kwa uchache Duniani.


Nae Mkuu wa wilaya ya Namtumbo Mh Ngolo Malenya ameipongeza kampuni ya uchimbaji madini MANTRA kwa kuichagua wilaya ya Namtumbo kwa kufanya uwekezaji huo yeye na wananchi wake kwa pamoja wapo tayari kutoa ushirikiano kwa MANTRA na anajivunia wilaya yake kua miongoni mwa wilaya itakayoenda kuchangia kipato kikubwa cha madini nchini.



Kwa upande wa mkurugenzi mtendaji wa MANTRA Ndg Alexandra akikabidhi kompyuta kwa Mkuu wa wilaya ya Namtumbo amesema kupitia uchimbaji madini ya Uranium utaenda kutoa fursa nyingi za ajira kwa wakazi wa Namtumbo na tayari wameshasainisha tenda kwa vikundi 11 vitakavyotoa huduma wakati mradi unaendelea na matarajio yao ni kuajiri watu wengi zaidi 


Aliongeza kwa kusema mradi huo unatarajiwa kuanza ujenzi rasmi mwaka 2026 na utagharimu takribani shilingi dola Billioni 1 hivyo wanategemea kuwepo kwa ongezeko kubwa la watu katika wilaya ya Namtumbo kutokana na kuwepo kwa fursa nyingi za ajira kwa wakazi wazawa na wageni watakaokuja kwenye wilaya hiyo.



Akizungumza kwa niaba ya Mbunge wa Namtumbo Vita Kawawa, Ndg Sharifu amesema anaishukuru serikali na Mh rais Samia Suluhu Hassan pamoja na wizara ya madini kwa kujali wananchi kwa kuwapa kipaumbele na kua wanufaika wa kwanza wa mradi huo na wanaahidi kutoa ushirikiano kwa wawekezaji MANTRA katika kipindi chote cha ujenzi wa mradi mpaka utakapokamilika.

   




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...