Na Said Mwishehe, Michuzi TV
KATIKA kuhakikisha sekta ya elimu inaendelea kuboreshwa, wadau muhimu wakiwemo Serikali Pamoja na watalaam wa kada mbalimbali nchini wameanza kufanya tathimini katika maeneo yaliyopewa kipaumbele kuona kama kuna changamoto ili zifanyiwe kazi kwa pamoja na hatimaye kufikiwa kwa malengo yaliyowekwa na serikali katika sekta hiyo nchini.
Wakati wa kikao kazi cha Kikosi Kazi cha kufanya tathimini kilichofanyika leo Septemba 19,2024 jijini Dar es Salaam wadau hao wamejadili masuala mbalimbali yenye lengo la kuboresha sekta ya elimu na miongoni mwa mambo yaliyojadiliwa ni uendelezaji wa taaluma ya ualimu, mazingira ya elimu, uwajibikaji na mpangilio mzuri wa ajira za wanataaluma hao .
Akizungumza wakati akifungua kikao kazi hicho Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Atupele Mwambene tayari kuna kikosi kazi cha pamoja kilichofanywa tathmini tangu mwaka 2022 na kuonyesha vipaumbele vya nchi katika sekta ya elimu na kufafanua tathimini hiyo ilihusisha mipango mbalimbali, kuona maeneo yenye changamoto au uhitaji.
Pamoja na mambo mengine amesema lengo ni kuhakikisha nchi inakuwa na lengo moja, makubaliano ya pamoja, vipaumbele vya pamoja na vyote viwe vya kuwezesha mabadiliko ya sekta ya elimu.
“Kinachokusudiwa ni kuona Tanzania inakuwa na afua za pamoja na kukubaliana kuandaa vipaumbe vya pamoja ili kufanikisha mabadiliko yanayotamaniwa kwa wadau kwa nyakati tofauti wamekuwa wakitoa maoni yao kuhusu umuhimu wa elimu yetu kuendelea kuboreshwa na Serikali imeamua kufanya maboresho hayo ikiwa sambamba na uwepo wa mitalaa mipya.”
Amesema kupitia tathimini hiyo sambamba na kuendelea kutatua changamoto, Imani yao ni kuwa sekta ya elimu itakuwa bora zaidi na kuongeza tathmini hiyo imehusisha wadau wa Serikali na wa maendeleo ya elimu na baadaye waliandaa andiko ambalo kufanikiwa kwake utatokana na ushirikiano wa wadau hao kufikia lengo.
Pia amesema kwa kuwa waliandaa Pamoja na ilihusisha afua ndani ya Serikali na wadau,hivyo utekelezaji wake unahitaji umoja na ndio maana leo Septemba 19,2024 wamekutana kwa ajili ya kufanya kutathmini namna ya kufanyia kazi makubaliano.
Aidha amesema kufanikiwa katika afua hiyo ya GPE, kunahitajika uhuishaji wa mipango iendane na mabadiliko ya sera ya elimu na mitalaa na kuongeza kwa kuwa kuna takwimu za sensa, uhuishaji pia unapaswa kufanyika ili kuingiza taarifa stahiki na sahihi zikiwemo zilizomo katika sensa ya watu na makazi.
Awali Stella Mayenge ambaye ni Meneja Programu Mwandamizi wa GPE kutoka Ubalozi wa Sweden,amefafanua kupitia mradi huo Tanzania ilinufaika awali kwa kupata fedha zaidi ya Sh.bilioni 228.3 na sababu za Tanzania kupata kiasi hicho kidogo ilitokana na kutotimiza baadhi ya masharti.
“Hivyo kinachofanyika sasa ni kuhakikisha inayatimiza masharti yaliyowekwa ili kutoa fedha hiyo ni kama Serikali ikiajiri walimu zaidi ya ule utaratibu wa kujaza nafasi tunawapa fedha.Masharti yaliyowekwa ni makubaliano kati ya wadau wanaosimamia GPE na Serikali.
Amefafanua lengo jingine na kufanyika kwa tathimini katika sekta ya elimu ni kuwezesha Tanzania kutimiza masharti yaliyobaki ili kupata fedha zote ambapo inaelezwa kama hayo masharti yatatekelezwa Serikali itanufaika na mradi wa Sh.bilioni 454.04 ambazo zinatolewa na Shirika la Ushirikiano wa Elimu Duniani (GPE).
Amesema sehemu ya masharti hayo ni uhuishaji wa takwimu za idadi ya watu, ambazo awali hazikuwa sawa kwa kuwa sensa haikuwa imefanyika, hivyo baada ya kufanyika kwa sensa ya watu na makazi inatakiwa kuwa na takwimu sahihi zitakazosaidia kuwa na mipango endelevu ya sekta hiyo.
Aidha amesema Pamoja na jitihada hizo bajeti ya Tanzania imekuwa ikishuka lakini wadau wanatamani kuona bajeti ipande hadi kufikia asilimia 20 ya bajeti nzima ya Serikali ielekezwe kwenye elimu.

Naibu Katibu Mkuu kutoka Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Atupele Mwambene akizungumza na Wadau wa Elimu leo Septemba 19,2024 Jijini Dar es Salaam wakati akifungua Mkutano wa kikao Kazi kilichokutana kufanya tatminini ya vipaumbele vilivyowekwa katika sekta ya elimu nchini
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...