Leo ni mwanzo wa Safari ya Baiskeli ya Twende Butiama 2024, safari ya kihistoria ambapo waendesha baiskeli 113, wakiwemo washiriki wa kimataifa kutoka Kenya, Rwanda, Congo, Malawi, Zambia, na Burundi, wanaanza safari ya kipekee ya kilomita 1,846 kutoka Dar es Salaam hadi Butiama. 

Waendesha baiskeli hawa watapitia mikoa 12 kati ya Septemba 29 na Oktoba 13, wakiwa na lengo la kuboresha maisha ya watu 100,000 watakaokutana nao njiani.

Msafara wa Twende Butiama umejikita katika historia ya Tanzania huku uliandaliwa kwa ajili ya kumuenzi Marehemu Mwalimu Julius Nyerere kwa vitendo. 

Kupitia kuendesha baiskeli- mchezo ambao Nyerere aliupenda- Twende Butiama inakusudia kupambana na maadui watatu wa maendeleo ya jamii: ujinga, umaskini, na maradhi.

 Huu ukiwa ni mwaka wake wa sita tangu kuanzishwa, msafara huu unaakisi fahari ya kitaifa, ujasiri, na dhamira thabiti ya kuwahudumia wananchi.Vodacom Tanzania imerejea kama mshirika mkuu kwa tukio la mwaka huu, ikipata msaada kutoka kwa wadau wengine kama Stanbic Bank Tanzania, YUNA, Kuunda, ABC Impact, na DarVelo Cycling. 

 Akizungumza wakati wa uzinduzi wa msafara huu, Zuweina Farah, mkurugenzi wa mahusiano na Vodacom Tanzania Foundation alisema, "Tunaamini katika kuleta maendeleo kupitia kuwawezesha watu na kutunza mazingira yetu.  

Mwaka jana, ushirikiano wetu na Twende Butiama ulifanikisha kupandwa miche ya miti 6,000, kuchangia madawati 610 kwa shule za msingi 13, na kutoa huduma za afya bure kwa zaidi ya watu 3,200 katika mikoa 3. Mwaka huu tumepata wadau wengine kuungana nasi kwa hivyo tuna Imani tutafanya mengi zaidi kuboresha maisha ya watanzania na kuenzi urithi wa Mwalimu.

”Msafara wa baiskeli ya Vodacom Twende Butiama ni  msafara wenye malengo makubwa. Waendesha baiskeli wanavuka kutoka pwani hadi Kaskazini mwa Tanzania huku wakijihusisha na huduma za kijamii katika nyanja za elimu, utunzaji wa mazingira, na afya kwa wote. 

Msafara wa mwaka huu unatarajia kuchangia madawati 1,500 kwa shule,ikiwa ni pamoja na kutoa msaada wa vifaa saidizi kwa shule zenye wanafunzi wenye mahitaji maalum. Msafara huu pia utapanda miche 50,000 sambamba na kutoa elimu ya utunzaji wa mazingita.

 Mwaka huu msafara huu utawezesha kutolewa kwa kambia za matibabu katika mikoa yote 12 watakapokatiza ambapo watu watapata huduma za ushauri, uchunguzi, na matibabu bure.Msafara wa Twende Butiama, uliyoanzishwa mwaka 2018 na wapenzi wa baiskeli wakiongozwa na Gabriel Landa, umekua kwa kasi, ukigusa maisha ya Watanzania wengi. 

Akizungumza kabla ya kuondoka, Landa alisema, "Msafara huu ni Zaidi ya kuendesha baiskeli, unahusu kurudisha kwa jamii na kuendeleza maadili ambayo Mwalimu alituachia. Kila kilomita tunayoendesha, tunaenzi falsafa yake ya kuboresha elimu, afya, na mazingira.

 Ni mchezo, lakini pia ni wito kwa wote kuchukua hatua kwa Tanzania bora.”Kile kilichoanza kama wito wa waendesha baiskeli wachache sasa kimekua kuwa jukwaa la kitaifa linalounganisha wadau tofauti chini ya lengo moja la maendeleo ya kijamii. 

Mbali na kusambaza vifaa vya shule, kupanda miti, na kutoa huduma za afya bure kwa maelfu, msafara wa mwaka 2024 wa Twende Butiama utaenda sambamba na   Digi-Truck itakayotoa mafunzo ya ujuzi wa kidigitali bure, shukrani kwa ushirikiano kati ya Huawei na Vodacom Tanzania.

 Annette Nkini meneja wa sustainability Stanbic Bank, alisisitiza kujitolea kwa benki hiyo kusaidia lengo hili muhimu, " Stanbic, tumejitolea kuwekeza katika miradi inayochochea maendeleo endelevu. 

Twende Butiama inaendana na lengo hili na inatoa fursa ya kuleta mabadiliko ya kudumu kwenye kuinua jamii, utunzaji wa kimazingira, kuchangia elimu na kuhakikisha kila mtu anapata huduma muhimu za afya.

"Kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita, msafara wa Twende Butiama umetoa mchango Chanya kwa jamii ya Watanzania, kutoka kuboresha miundombinu ya shule hadi kukuza uendelevu wa mazingira.

 Waendesha baiskeli wanapoelekea Butiama, wataendelea kuenzi urithi wa Nyerere, kuhamasisha vizazi vijavyo, na kuimarisha roho ya umoja na fahari ya kitaifa.


Mama Maria Nyerere (centre), Mke wa Hayati Julius Kambarage Nyerere, akizungumza na msafara wa Twende Butiama 2024 walipomtembelea nyumbani kwake Msasani Dar es Salaam kabla ya kuanza rasmi safari ya kutoka Dar es Salaam mpaka Butiama tarehe 29 Septemba 2024. Kuanzia kushoto ni Gabriel Landa, Mwanzilishi wa Twende Butiama, Gertrude Mongella na Zuweina Farah, Mkurugenzi wa  Vodacom Tanzania Foundation ambao ndio wadhamini wakuu wa msafara huo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...