Waziri wa Maji Jumaa Aweso, amewahakikishia wananchi wa wilaya ya Mbinga na Nyasa, kupata huduma ya maji safi na salama kutokana na miradi ya maji  inayotarajiwa kukamilika hivi karibuni chini ya Wakala wa maji safi na mazingira Vijijini RUWASA  katika wilaya hizo.


Ameyasema hayo leo katika ziara yake wilayani Nyasa na Mbinga Mara baada ya kutembelea miradi ya Tingi-Malungu, Miyangayanga pamoja na Matiri, amesema katika kipindi chote ambacho ataiongoza Wizara ya maji hatakuwa kikwazo kwa wananchi hao kupata huduma bora ya maji safi na salama.



Amesema maendeleo ni mchakato na ili kufikia adhima hiyo ni lazima kuwepo na ushirikianao baina ya watendaji wa wizara ya maji pamoja na taasisi zingine hivyo kama wizara wanajukumu lakuhakikisha wanaendelea kushirikiana vyema pamoja kwani wizara hiyo sio ya ukame ambapo watahakikisha maji yanapatikana ya uhakika.


Waziri Aweso ameeleza kuwa kwa asilimia kubwa wanaoteseka na changamoto ya maji ni kinamama hivyo amewaagiza watumishi wa wizara ya maji  kuhakikisha watu wenye shida ya maji wanapatiwa huduma hiyo.



Amebaisha kuwa kiasi ya milioni 170 kimetolewa kwaajili ya kusambaza mabomba ya maji Miyangayanga Wilayani Mbinga, na milioni 100 kusambaza mabomba ya maji kijiji cha Tingi, pamoja na kiasi cha milioni 145 kutolewa kwaajili ya kumlipa mkandarasi wa mradi wa Songambele.


Akizungumza Mbunge wa Nyasa Eng. Stella Manyanya, amesema kulikuwa na changamoto kwa kinamama wakati wa kujifungua ambao walilazimika kwenda mtoni kuchota maji, huku wengine wakiingia katika migogoro ya kugombania maji katika maeneo ambayo yalikuwa na maji, jambo ambalo lilimlazimu kutumia gharama zake binafsi kutafuta ahueni kwa kuchimba visima hivyo kupitia mradi huo mkubwa utakwenda kuondoa adha ya upatikanaji wa maji katika vijiji hivyo.



Kwa upande wa Mbunge wa Mbinga Mjini Jonas Mbunda ametoa pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassani pamoja na wizara ya Maji kupeleka mradi wa maji kwenye jimbo lake huku matumaini yake nikwenda kuondoa changamoto zilizokuwepo kwa wananchi wake kutembea umbali mrefu kufuata huduma hiyo.


Imeelezwa kuwa mradi wa Tingi-Malungu unatekelezwa na mkandarasi Peace Construction Limited ambao umegharimu kiasi cha Bilioni 1.2 na unatarajia kuhudumia wanakijiji zaidi ya  elfu 9600, na unaotarajiwa kukamilika tarehe 30 oktoba mwaka huu, huku mradi wa maji Matiri umegharimu kiasi cha Bilioni 1.6 ambao umefikia asilimia 98 ya utekelezaji.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...