Na Mwandishi Wetu
WAZIRI wa Afya Jenista Mhagama amesema anamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na Serikali ya Uingereza kwa kuamua kufanya kazi ya kutokomeza magonjwa haya amabyohayapewi kipaumbele.
Ametoa shukrani hizo Septemba 18, 2024 wakati wakiwa katika ziara pamoja na Princess Sophie (Duchess of Edinburgh) ambae ni Mke wa Mtoto wa Mfalme wa Uingereza walipotembelea Kituo Cha Afya cha Mlandizi mkoani Pwani kwa lengo la kujionea utoaji huduma za matibabu ya macho
"Yapo magonjwa ambayo hayajapewa kipaumbele sio Tanzania tu bali
Duniani kote ikiwemo ugonjwa huu wa macho ( Trakoma) lakini pia magonjwa kama mabusha, matende, minyoo ya tumbo, kichocho."
Aidha ametoa ra kwa Watanzania hasa wa Mkoa wa Pwani kushirikiana na Serikali kumhamasisha mwananchi yeyote mwenye dalili za ugonjwa wa macho kwenda
hospitali kwani ugonjwa huo husababisha upofu.
Kwa upande wake, Princess Sophie (Duchess of Edinburgh) amesema lengo la Uingereza ni kuhakikisha Tanzania inatokomeza magonjwa yasiyopewa Kipaumbele.
"Haya yote yanawezekana kupitia ushirikiano ambao tunautoa kwa Tanzania ikiwa ni kwa mtu mmoja mmoja katika kutokomeza magonjwa ya trakoma,"amesema Sophie na kusisitiza kwa pamoja wanaweza kutokomeza ugonjwa huo wa
trakoma.
wa matibabu ya ugonjwa wa trakoma yanayotolewa na Serikali kupitia
Wizara ya Afya kwa kushirikiana na wadau akiwemo Sightsavers.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...