WAZIRI wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe.Jerry Silaa amewaomba viongozi wa kanisa kuwaasa waumini wao kutenga muda wa kujiandikisha katika daftari la wapiga kura ili wapate nafasi ya kushiriki kuchagua viongozi kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Ombi hilo amelitoa leo Septemba 29,2024 katika harambee ya ujenzi wa kanisa la KKT Kigezi-Chanika Jijini Dar es Salaam.
Aidha amesema waumini wa kanisa wanaweza pia kuomba nafasi za uongozi,kwa lengo la kupata viongozi wenye hofu ya mungu ili kuleta maendeleo bora na ustawi wa jamii.
Pamoja na hayo amesema jukumu la uraia linajumuisha kuchagua na kuchaguliwa kuwa viongozi kwa ajili ya wananchi wote ambapo upatikanaji wa huduma ya shule, zahanati na mengine yanahusiana na uwepo wa viongozi wanaopatikana kupitia chaguzi.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...