Na. Vero Ignatus, Arusha

Airtel imechukua jukumu la kudhamini mchezo wa Golf kila mwisho wa mwezi wa Monthly Mug kwa kushirikiana na club ya gymkhana ambapo Vijana wameaswa kujiunga na kuondoka kwenye Dhana kwamba mchezo huo ni wa Wazee na Matajiri.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Arusha Mkurugenzi wa biashara kutoka Airtel makao makuu Joseph Muhere amesema wanechukua jukumu la kudadhili mchezo huo kila mwisho wa mwezi mashindano ili kuhamasisha kufahamika zaidi kwa mchezo huo.

Muhere amesema wameamua kufanya hivyo kwasababu mchezo huo ili kuhamasisha kukua kwani Golf ni mchezo mahususi na wenye heshima kubwa duniani, Ila ni musukumo kwa wa Tanzania wengi kujiunga na kuwaleta watu pamoja ili kuufahamu mchezo huo zaidi

"Watu wengi ukiongelea michezo wanajua tu Mpira wa miguu, bila kujua Golf ni mchezo Mahususi na wenye heahima Sana popote duniani unafahamika, wa Tanzania jiungeni na club hii yapo matawi mengi Ila Sisi tumeanzia Arusha"

Muhere wao kama Airtel Tanzania dhumuni Kuu kuwaleta watu kuudhamini mchezo kwani sehemu muhimu ya kukutana na watu wengi wenye family tofautitofauti, kujadili Mambo ya biashara, uchumi na maendeleo kwa ujumla

vilevile mchezo huo ni Ajira, kukuza vipaji kujenga Afya hivyo mtu ukifuata utaratibu ni mchezo kama ilivyo michezo mingine

"Ukijifunza utaelewa Mimi nilikuwa sijui kucheza nimefundishwa na sasa nauelewa , hivyo Airtel tu me kuwa balozi wa kuwapelekea tasrifa vijana na watu wengi juu ta mchezo huu, siyo mchezo wa matajiri, wazee hapana ni kufuata tu utaratibu waweze kuendeleza vipaji

Akizungumza Mara baada ya kushiriki mashindano hayo Golf Paul Mattysen katika mashindano ya Macklymarc ambao ni mchezo unaochezwa kila mwisho wa mwezi ambapo umefadhiliwa na Airtel ambapo waoikuwa wachezaji wapatao 36

Amesema kama mchezaji wa siku nyingi zipo moja ya faida ni pamoja na kujiweka sawa kimwili huku akiwataka wazazi kuwashauri vijana kujiunga na mchezo huu wa Golf japokuwa ni mchezo wa gharama Ila kwa udhamini wa Airtel vijana wachangamkie fursa hiyo

Tunaiomba Airtel iwanunulie vijana vifaa vya Golf kwani Kununua golf kit ni siyo chini ya dola 1500 karibia mil 4 na kuna vitu vingine bado "Inasikitisha vijana hawataki kucheza golf kwani wachezaji wengi hodari duniani ni vijana Sisi wazee tunapita hakuna vijana wa kuwaachia huu mchezo sasa". Alisema mchezaji huyo wa siku nyingi

Kwa upande wake meneja mashindano kutoka klabu ya Gymkhana Jijini Arusha Abass Lalji amesema udhamini wa Airtel katika mchezo huo utaongeza hadhi ya Golf kwenye klabu hiyo

" Mchezo huu wanacheza watoto watu wazima vilevile wanawake wanacheza inategemea na utayari wa mtu" Alisema.
Mkurugenzi wa biashara kutoka Airtel makao makuu Joseph Muhere akizungumzia namna ambavyo wameamua kudhamini mshindano ya Golf ya monthly Mug kwa kushirikiana na Klabu ya Gymkhana Jijini Arusha
Mmoja wa washiriki katika mashindano ya mchezo wa Golf kila mwisho wa mwezi wa Monthly Mug kwa kushirikiana na Klabu  ya Gymkhana
Katika picha baadhi ya wafanyakazi wa Airtel TANZANIA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...