Benki ya KCB nchini Tanzania Yapanda Miti Katika Mikoa Minane Nchini Tanzania kwa Kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja.

KCB inaongoza juhudi za maendeleo endelevu kama kampuni inayowajibika kwa jamii, kwa kuendeleza Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) 14 kupitia mkakati madhubuti unaojikita katika nguzo za kiuchumi, kijamii, na kimazingira.

Kwa kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja, KCB Bank ikiwakilishwa na Paschal Machango kwa niaba ya Cosmas Kimario, Mkurugenzi wa Biashara wa Kanda wa KCB Group na Mkurugenzi Mtendaji -KCB Bank Tanzania, imechukua hatua muhimu ya Kimazingira kwa kupanda miti zaidi ya 1,500 katika mikoa mbalimbali ya uendeshaji wake nchini Tanzania.

Wakati wa hafla hiyo, Machango alitoa shukrani kwa Shule ya Msingi Mbagala Annex, moja ya wanufaika wa mpango huo, kwa kuipokea KCB Bank kwa moyo mkunjufu katika juhudi hii muhimu ya kuhifadhi mazingira.

“Dhamira yetu inakwenda zaidi ya mafanikio ya kibiashara; tumejikita katika uhifadhi wa mazingira.

Leo hii, tunajivunia kupanda zaidi ya miti 1,500 katika shule mbalimbali zilizoko Dar es Salaam, Arusha, Kilimanjaro, Zanzibar, Geita, Kahama, Mwanza, na Morogoro,” alisema Machango.

Naye Ruth Mussa, Mwalimu Msaidizi wa Shule ya Msingi Mbagala Annex, alitoa shukrani zake kwa KCB Bank kwa kushiriki katika mpango huo, huku Afisa Mazingira wa Manispaa ya Temeke, Phina Bernad, akiipongeza benki hiyo kwa mchango wake mkubwa na kusisitiza umuhimu wa kuhakikisha miti iliyopandwa inatunzwa ipasavyo.

Aidha KCB inatoa wito kwa jamii na mashirika kushirikiana katika kuendeleza juhudi za kuhifadhi mazingira na kufikia maendeleo endelevu kwa manufaa ya vizazi vijavyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...