Na Mwandishi Wetu


Hospitali ya CCBRT iliyoko Msasani Dar es Salaam inaungana na dunia kuadhimisha siku ya afya ya macho duniani mwaka 2024, kwa kusogeza huduma za macho karibu na watanazania wenye mahitaji, ambapo hospitali hiyo inaendesha zoezi la upimaji wa afya ya macho kwa wakazi wa Tegeta na maeneo ye Jirani bila malipo.

Sambamba na hilo, siku za hivi karibuni hospitali hiyo imefungua duka jipya la miwani katika jengo la Kibo Complex Tegeta, kwa lengo la kuwafikishia huduma hiyo muhimu wananchi wa maeneo hayo.

Kauli mbiu ya afya ya macho kwa mwaka huu inahimiza vijana na watoto kupenda macho yao na kuitaka dunia kuongeza umakini katika upatikanaji wa huduma bora za macho kwa vijana.

Daktari Cyprian Ntomoka, ni bingwa wa magonjwa ya macho katika hospitali ya CCBRT anafafanua kuwa, “Siku hii sio tu imetengwa kwa ajili kuhamasisha bali pia inalenga kuwasaidia watu kuchukua hatua za dhati za kutunza afya ya macho yao. CCBRT inalenga kutoa huduma zinazokidhi mahitaji ya rika tofauti katika jamii yetu, kuhakikisha kila mtu anapata huduma muhimu za macho. Hii ndiyo sababu, katika maadhimisho haya, tunafanya uchunguzi wa macho bure wa siku mbili tarehe 9 na 10 Oktoba 2024 nje ya jengo Kibo Comlex Tegeta, ambapo siku za hivi karibuni tumefungua duka jipya la miwani.”

Katika duka la Miwani la CCBRT Tegeta Kibo Complex utaweza kujipatia miwani kwa ajili ya matumizi ya computer na simu, mwani ya jua, miwani ya kuendeshea gari na ile ya kusomea.

Pamoja na matibabu ya magonjwa mengine hospitali ya CCBRT kwa miaka zaidi ya 30 imekuwa kinara wa utoaji wa huduma bora za afya ya macho hapa nchini ambapo huduma hizo hujumuisha, huduma za macho za jumla yaani , Kliniki ya macho kwa kila siku ambapo hufanya uchunguzi wa macho, utambuzi, na matibabu ya magonjwa mbalimbali ya macho na kuhakikisha huduma kamili kwa wagonjwa wa rika zote.

Huduma nyingine ni huduma za macho kwa watoto ambapo CCBRT hutoa matibabu ya matatizo mbalimbali ya macho kwa watoto, ikiwemo kurekebisha makengeza kwa njia ya upasuaji au miwani na hivyo kuboresha afya ya macho ya watoto na kuwaondolea unyanyapaa kutoka kwa wenzao kutokana na kuwa na macho yenye muonekano tofauti.

Matibabu ya pazia ya nyuma ya jicho pia hotolewa katika hospitali hiyo ambapo wataalamu wa CCBRT kwa kutumia vifaa vya kisasa wanaweza kutambua na kutibu magonjwa ya jicho nyuma ya pazia ambayo wakati mwingine husababishwa na magonjwa kama vile kisukari, presha ya macho, umri mkubwa au kuumia kwa jicho kutokana na ajali au kitu chochote.

Miwani ni sehemu ya matibabu ya jicho hivyo miwani na lenzi za kisasa zenye ubora wa hali ya juu hupatikana katika maduka ya miwani ya CCBRT Msasani na Tegeta Kibo Complex.

Huduma za Macho ya Bandia: Kwa watu waliopoteza jicho, pia hotolewa katika hospitali ya CCBRT Msasani na na hivyo kumrejeshea muhusika muonekano mzuri na kujiamini.

“Kauli mbiu ya mwaka huu inatutaka wote tulinde afya ya macho yetu lakini imeenda mbali ikatutaka tulinde afya ya macho kwa watoto. “Nitumie fursa hii kuwakumbusha tena wazazi na walezi wenzangu matumizi yasiyokuwa na mipaka ya vifaa vya elektroniki kama vile simu, kompyuta, televisheni na vingine vingi vyenye mwanga mkali vinaweza kuhatarisha afya ya macho ya watoto wetu. Nasisitiza umuhimu wa kulinda macho ya watoto ili kuzuia matatizo ya kuona yatokanayo na matumizi ya vifaa hivi”, alionya Dk Ntomoka.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...