ALIYEKUWA Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi kupitia jimbo la Vunjo wilayani Moshi mkoani Kilimanjaro, Liberat Mchau ametimkia Chama cha Mapinduzi na kupokelewa na Katibu wa CCM mkoa wa Kilimanjaro, Mercy Mollel katika mkutano wa Chama jimbo la Vunjo.

Mchau alisema kuwa, lengo la kutimkia CCM ni baada ya kuridhishwa na utendaji kazi wa Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Chama cha Mapinduzi.

"Yale yote ambayo tulikuwa tukipambana nayo huko nyuma na kuyasema majukwaani ili Serikali iyafanyie kazi Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na Serikali yake imeyatekeleza kwa vitendo sasa nikajiuliza kwanini nisije kumuunga mkono kwa vitendo" Alisema Mchau.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...