-Yaingia mtaani kusikiliza na kutatua changamoto za kihuduma

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) imeanza maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja kwa kuwafikia wateja wake katika maeneo mbalimbali ya kihuduma katika Mikoa ya Dar es salaam na Pwani ili wanatatua na kuboresha huduma.

Akizungumza na vyombo vya habari , Mkurugenzi wa Huduma kwa wateja DAWASA, CPA (T) Rithamary Lwabulinda ameeleza kuwa kwa kipindi chote cha maadhimisho Watumishi wa Mamlaka watakuwa katika mitaani kusikiliza, kupokea na kutatua changamoto mbalimbali za kihuduma zinazowakabili ili kuhakikisha kila mwananchi anapata huduma bora.

"Wiki hii ni muhimu sana katika usimamizi wa utoaji huduma kwani itasaidia kuimarisha mahusiano baina ya Mamlaka na wateja wake, lakini zaidi kuwafikia Wananchi katika makazi yao na kupata majibu, maoni na mapendekezo yanayosaidia kuboresha huduma yetu" ameelza Bi.Lwabulinda.

Kwa upande wake, ndugu Hashim Ally mkazi wa Kisarawe ameipongeza DAWASA kwa kufika mtaani na kuwasikiliza kwani itasaidia kuboresha huduma na kuchagiza mahusiano chanya kati ya wateja na Taasisi.

Wiki ya huduma imebeba kauli mbiu isemayo "Ni zaidi ya matarajio" huadhimishwa tarehe 7 - 11 mwezi Oktoba kila Mwaka.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...