Na Humphrey Shao
Mkuu wa Wilaya Ilala Edward Mpogolo leo emeongoza wakazi wa Wilaya hiyo katika zoezi la uandikishaji katika Daftari la Makazi kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa unataraji kufanyika Novemba 27, 2024..
Mara baada ya Kujiandikisha DC Mpogolo alipata furs ya kutembelea Vito vingine Luna hali YA zoezi hilo ambapo ametembelea Vituo vya Ilala, Upanga na Buguruni
Aidha DC Mpogolo ametoa wito kwa wakazi wa Ilala kujitokeza kujiandikisha mapema na kuacha kusubiri mwishoni na hili wajipange katika foleni na misululu ya muda mrefu.
Waziri wa nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI ) Mhe. Mohamed Mchengerwa aliutangazia Umma wa Tanzania na Vyama vya siasa kuwa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Tanzania Bara utafanyika tarehe 27 Novemba, 2024
Waziri Mchengerwa alieleza hayo leo tarehe 15 Agosti, 2024 wakati akitoa Tangazo la Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na kuzindua nembo rasmi ya uchagunzi wenye kaulimbiu isemayo " Serikali za Mitaa, Sauti ya Wananchi, Jitokeze kushiriki ".
"Ninautangazia Umma wa Watanzania na Vyama vyote vya Siasa vyenye Usajiri wa kudumu kuwa tarehe 27 Novemba, 2024 itakuwa siku ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Tanzania Bara, Upigaji wa kura utaanza saa mbili kamili za Hasubuhi nakukamilika saa kumi kamili za jioni" alisema mchengerwa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...