Karama Kenyunko Michuzi Tv 

DEREVA wa Mamlaka ya Bandari Tanzania, TPA Tino Ndekela na wenzake saba, wamefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na jumla ya  mashtaka 20 ikiwemo utakatishaji wa zaidi ya Sh. Bilioni 20 na kuisababishia Kampuni ya Kimataifa ya Kuhifadhi Mafuta (TIPER) Tanzania hasara ya Sh. Bilioni 26.

Katika kesi hiyo, washtakiwa wanakabiliwa na mashta nane ya wizi wa zaidi ya Lita Milioni 6.3 za  mafuta ya diesel,  na mashtaka nane ya wizi wa zaidi ya  lita milioni 3.5 za wa mafuta aina ya Petrol mali ya Tiper. 

Mashtaka mengine yanayowakabili washtakiwa ni uharibifu wa  wa mali kwa lengo la kutoa huduma ya zaida, Utakatishaji na shtaka moja la kuisababishia Tiper hasara.

Katika hati ya mashtaka iliyosomwa mahakamani hapo na wakili wa serikali  Cathebert Mbilingi mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Beda Nyaki, imewataja washtakiwa wengine kuwa ni Fikiri Kidevu, Amani Yamba, Mselem Abdallah Kika Sanguti, Twaha Salum,  Audience Shayo, Hamis Hamis

Akisoma hati ya mashtaka, Mbilingi amedai kuwa kati ya Januari 2019 na Desemba 2022 huko Tungi katika Wilaya ya Kigamboni jijini Dar es Salaam, washitakiwa waliaribu miundombinu ya  bomba la kusafirishia mafuta ya  Disel na Petrol Mali ya Tiper.

Katika kosa la wizi inadaiwa siku na mahali hapo katika nyakati tofauti, washtakiwa wote waliiba mafuta hayo ya Diesel na Petrol mali ya Tiper.

Imeendelea kudaiwa kuwa,  Kati ya January Mosi na Desemba 2022 huku Tungi katika Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, washtakiwa kwa makusudi waliisababishia Tiper hasara ya Sh. 26,019,047,803.99.

Wakili Mbilingi amedai kuwa, kipindi hicho hicho katika mkoa wa Dar es Salaam na Pwani, washtakiwa walijipatia kiasi cha Sh. 20,huki wakijua kuwa fedha hizo ni zao la kosa la wizi.

Hata hivyo washtakiwa hawakuruhusiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchumi ambazo kwa kawaida husikilizwa mahakama Kuu ama kwa kupewa kibali kutoka kwa DPP. 

 Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika na kesi imeahirishwa hadi Novemba 4,2024. Washtakiwa wote wamerudishwa rumande. 

Baadhi wa washtakiwa wa wizi katika Kampuni ya Kimataifa ya Kuhifadhi Mafuta Mafuta (TIPER) wakirudishwa mahabusu mara baada ya kumaliza kusomewa kesi yao yenye mashtaka 20



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...