KAMPUNI ya Itel Tanzania imekabidhi msaada wa bidhaa mbalimbali katika Shule ya Msingi Tandale, wilayani Kinondoni, Dar es Salaam, ikiwa ni hatua ya kurejesha pato lake  kwa wananchi.  


Msaada huo ni pamoja na Kompyuta tatu,viti kwaajili ya ofisi ya walimu, vitabu vya wanafunzi, madaftari,mabegi,taulo za kike, vifaa vya michezo na zawadi mbalimbali kwa wafunzi.



Akikabidhi msaada huo, Ofisa Uhusiano wa Itel Tanzania ,Sophia Msafiri, amesema ni utaratibu wa kampuni hiyo kurejesha pato lake kwa jamii hususan shule, watoto wenye mahitaji maalumu na kushiriki shughuli za kijamii.


“Itel Tanzania leo tumechagua kutoa zawadi katika Shule ya Msingi Tandale..Ni kawaida yetu  kusaidia shule za msingi na sekondari. Pia tunasaidia  vituo vya yatima na shughuli za kijamii,”amesema Sophia.



Sophia amesema kampuni hiyo itaendelea kuunga mkono jamii kupitia utaratibu huo wa kurejesha faida inayopata.


Mwalimu Mkuu wa Shule ya 

Msingi Tandale,Andrew John, ameishukury Itel Tanzania kwa maaada huo na kueleza utasaidia utoaji wa elimu.



Amesema shule hiyo inazaidi ya wanafunzi 2000 na inaongoza kwa kufaulisha wanafunzi  wilayani Kinondoni, hivyo msaada huo utaongeza ufanisi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...