NA VICTOR MASANGU, KIBAHA

Halmashauri ya mji Kibaha iliyopo Mkoa wa Pwani katika kukuza na kuinua kiwango cha elimu imetekeleza kwa vitendo maelekezo ya Rais wa awamu ya sita Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kukabidhi madawati 4000 katika shule za msingi 46 na sekondari 20 ambayo yatakuwa ni mkombozi mkubwa kwa wanafunzi kuondokana na kero na changamoto ya wanafunzi kukaa chini na kusoma kwa mlundikano.

Akikabidhi Madawati hayo Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka katika halfa iliyofanyika katika shule ya msingi Mkoani na kuhudhuliwa na viongozi mbali mbali wa chama na serikali amesema kwamba lengo kubwa la serikali ya awamu ya sita ni kuhakikisha kwamba inaweka mipango madhubuti kwa ajili ya kuwawezesha wanafunzi waweze kusoma katika mazingira ambayo ni rafiki.

Koka alisema kwamba uwepo wa madawati hayo kutakwenda kumaliza changamoto ya wanafunzi kusoma katika hali ya mlundikano na kwamba wanafunzi hao wataongeza kasi ya hali ya kiwango cha ufaulu kutokana na kusoma wakiwa wamekaa katika madawati bila ya kulundikana.

Pia Mbunge huyo aliupongeza uongozi wa Halmashauri ya mji Kibaha kwa kuweka mikakati ya kuamua kununua madawati hayo elfu 4000 kupitia makusanyo yao ya mapato ya ndani ili kumaliza kero za wanafunzi ambazo zilikuwepo katika baadhi ya shule za msingi na sekondari ya kuwa na uhaba wa madawati.

"Kwa kweli napenda kuchukua fursa hii ya kipekee katika kuwapongeza viongozi mbali mbali wa chama pamoja na serikali wakiongozwa na Rais wetu mpendwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuweza kutenga fedha nyingi katika maeneo mbali mbali ndani ya Jimbo la Kibaha katika sekta ya elimu ambazo zimekwenda kujenga hata shule mpya za msingi na sekondari.

Alifafanua kwamba sekta ya elimu ndio ufungua wa maisha na kwamba ataendelea kushirikiana bega kwa bega na wananchi pamoja na serikali katika kuboresha sekta ya elimu ikiwemo miundombinu ya vyumba vya madarasa sambamba na kuongeza zaidi viti na meza ili wanafunzi waweze kusoma bila changamoto yoyote.

Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya mji Kibaha Dkt.Rogers Shemwelekwa amesema kwamba mpango wa kununua madawati hayo ni maelekezo ya Rais wa awamu ya sita Dkt. Samia Suluhu Hassan ili kuweza kuboresha sekta ya elimu na kuwaondolea na kitatua kero za wanafunzi kusoma katika mazingira magumu.

Aidha alisema kwamba kwa sasa Halmashauri ya mji Kibaha ina jumla ya shule zipatazo 66 za serikali ambapo kati ya hizo shule za msingi ni 46 na shule za sekondari zikiwa ni 20 zenye jumla ya wanafunzi wapatao 17,424.

"Tumekabidhi madawati yapatayo 4000 ambayo yatakwenda katika shule za msingi 46 na mengine tutagawa katika shule za sekondari 20 ikiwa ni moja ni moja ya utekelezaji wa maelekezo ya Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha wanasoma katika mazingirarafiki na kuondokana na kero za kusoma katika mlundikano," alisema Shemwelekwa.

Kadhalika mkurugenzi huyo aliongeza kwamba hali ya uboreshwaji wa miundombinu ya madarasa 217 pamoja na matundu ya vyoo tayari yameshajengwa na kwamba wanaendelea kutekeleza maelekezo ya Rais Samia ambapo wamefanikiwa kutengeneza madawati 2,100 kwa shule za msingi pamoja na viti na meza 2,000 kwa shule za sekondari.

Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji Kibaha Mussa Ndomba amesema kwamba kitu kikubwa ambacho wamejiwekea kama madiwani ni kuhakikisha wanatatua kero katika nyanja mbali mbali ikiwemo kuboresha sekta ya elimu ili kuweza kuongeza kasi ya kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi.

Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Nickson Simon hakusita kuipongeza kwa dhati halmashauri ya mji Kibaha kwa kuweka mipango mikakati ya kuongezeka kwa kasi ya ukusanyaji wa mapato ambao ndio umepelekea kupatikanika kwa fedha ambazo zimeweza kununua madawati hayo elfu 4000 ambayo yatasambazwa katika shule za msingi pamoja na sekondari.







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...