Wafanyabiashara wa chakula maarufu kama 'Mama Lishe' wameeleza shukrani zao kwa Kampuni ya Coca-Cola kwa kuanzisha wazo bunifu kupitia tamasha la 'Coca-Cola Food Fest', ambalo limekuwa chachu ya kuboresha maisha yao kiuchumi.
Akizungumza wakati wa tamasha hilo, Veronica Athanas, mmoja wa Mama Lishe, alisema, "Matamasha kama haya yanatupa fursa ya kujifunza na kuboresha biashara zetu, na kwa hakika yamechangia kuongeza kipato chetu."
Asha Mohammed, mwenzake, aliongeza, "Tamasha hili limetufundisha mbinu za kisasa za kuendesha biashara zetu, na tunatoa wito kwa wadau zaidi kujitokeza kusaidia juhudi hizi muhimu."
Wafanyabiashara hao waliishukuru Coca-Cola kwa kuandaa tamasha hilo lenye manufaa, wakisisitiza kuwa limewapatia maarifa mapya ya kuboresha biashara zao. Aidha, walitoa wito kwa sekta mbalimbali kuwekeza zaidi katika kusaidia wafanyabiashara wadogo kama wao, kwani msaada huo utaimarisha si tu biashara zao, bali pia uchumi wa familia na jamii kwa ujumla.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...