Msafara wa kihistoria wa Vodacom Twende Butiama 2024 umekamilika rasmi mnamo tarehe 13 Oktoba kwa mafanikio makubwa, ukihitimishwa wilayani Butiama, kijijini kwa Hayati Baba wa Taifa, Mwl. Julius K. Nyerere katika mkoa wa Mara. 

Msafara huo, uliowakutanisha waendesha baiskeli zaidi ya 100 kutoka Tanzania na nchi jirani, ulifanyika kuanzia tarehe 29 Septemba na kupita katika mikoa 12 ya Tanzania.

Mafanikio ya msafara huu ni pamoja na kutoa huduma za afya bure kwa maelfu ya wananchi katika kambi za matibabu zilizowekwa njiani. Zaidi ya madawati 1000 yalichangwa kwa shule mbalimbali, zikiwemo shule zinazohudumia wanafunzi wenye mahitaji maalum, huku miche 50,000 ya miti ikipandwa katika maeneo mbalimbali ambako msafara huu ulipita, lengo likiwa kuhifadhi mazingira.

Ubunifu huu wa Msafara wa Vodacom Twende Butiama, ulianzishwa mwaka 2018, umeendelea kuwa jukwaa muhimu la kusaidia jamii kupitia utoaji wa huduma za kijamii katika nyanja za elimu, afya, na mazingira.








 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...